• HABARI MPYA

    Monday, October 15, 2012

    TOLEO LA KATI, LA MWISHO WA VITUKO SHOW WAREKODI WIMBO WA R&B



    Toleo la Kati na Tabitha

    Toleo la Mwisho amekumbatia Tabitha

    Wakiwa na 'mke wao' Tabitha

    Utapenda swaga zao

    Kipa wa Coastal Union, Jackson Chove akimpima uzito Tabitha

    Chove na Tabitha

    Juu ni Mze Jangala na Lulu na chini huku ni makachaa watatu
    Na Mahmoud Zubeiry
    WASANII wa kundi la Vituko Show la Tanga, Kazi Suleiman ‘Toleo la Kati’ na Ally Bofu ‘Toleo la Mwisho’, kwa kushirikiana na Chamoyo, wametoa wimbo uitwao Mamido, ambao muda si mrefu utaanza kusikika kwenye vituo mbalimbali vya Radio nchini.
    Toleo la Kati, aliiambia BIN ZUBEIRY jana kwamba, wimbo huo wamerekodi katika studio za Gizzle Records mjini Tanga na wako mbioni kuufanyia video, wakiwashirikisha wasanii wenzao wa Vituko Show, kama Lulu Matawalo ‘Baby Brown’ na Tabitha Jacob ‘Mama Shotii’.
    “Hii ngoma brother imesimama sana, we utaisikia ikitoka, tumepiga mtindo wa R&B, yaani tumeharibu vibaya,”alisema Toleo la Mwisho.
    Kwa nini wanajiita Toleo la Kati na la Mwisho; “Unajua Mungu katika kuumba walemavu, mimi ni toleo la mwisho kabisa la walemavu, na mwenzangu (Kazi), yeye ni toleo la kati,”alisema Ally Bofu.   
    Kundi la Vituko Show linaloongozwa na magwiji wa sanaa ya uigizaji nchini, kama Mzee Jangala na King Majuto, limejizolea sifa za kutosha ndani ya muda mfupi, kutokana na kuibua wasanii wakali kama Kitale na Sharo Milionea. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: TOLEO LA KATI, LA MWISHO WA VITUKO SHOW WAREKODI WIMBO WA R&B Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top