Hiki ni kikosi cha Mseto FC ya Morogoro mwaka 1990, wakati
huo inashiriki Ligi Daraja la Pili, ambayo sasa ni Daraja la Kwanza. Mseto imewahi
kuwa bingwa wa Tanzania mwaka 1975. Sasa hivi timu hii haipo kabisa katika
ramani ya soka nchini. Timu nyingine maarufu mkoani Morogoro kama Tumbaku na
Reli, ambazo pia ziliibua vipaji vya nyota wengine wengi nchini enzi hizo, nazo
pia zimepotea katika ramani ya soka. Kweli majanga!