Ziara ya
mwanasoka bora wa zamani Afrika, Abedi Ayew Pele katika makao makuu ya klabu ya
Azam, Azam Complex jana, itaonyeshwa leo katika kipindi cha Azam FC TV Show,
kinachorushwa hewani kupitia Televisheni ya Channel Ten, kuanzia Saa 3:00 usiku
leo. Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa Meneja wa Azam, Patrick Kahemele. Pichani ni King Pele akiwa na mshambuliaji wa Azam Academy, Jamil Balotelli jana.
|