• HABARI MPYA

    Saturday, February 09, 2013

    ARSENAL YASHINDA IKIPATA PIGO


    KIUNGO wa Arsenal, Jack Wilshere alijikuta anaumia wakati timu yake ikishinda 1-0 dhidi ya Sunderland baada ya kugongana na Alfred N'Diaye.
    Haikuonekana kama kuwa pigo kubwa kutoka kwa mchezaji huyo mpya wa Sunderland, lakini lilitosha kumfanya Wilshere atoke uwanjani akimpisha Abou Diaby.
    Down: Jack Wilshere was in distress when receiving treatment after the collision
    Jack Wilshere akigulia maumivu wakati akitibiwa
    Awali ya hapo, Laurent Koscielny, ambaye alipangwa kwenye kikosi cha kwanza cha Arsenal leo, ilibidi aondolewe baada ya kuumia wakati wa kupasha misuli moto kujiandaa na mchezo huo.
    Alifaulu vipimo vya maumivu kabla ya mechi, lakini hakuweza kucheza maana yake Bacary Sagna ilibidi acheze beki ya kati na Carl Jenkinson akaanza beki ya kulia.
    Arsenal pia ililazimika kucheza dakika 30 za mwisho bila Carl Jenkinson, ambaye alitolewa nje kwa kadi ya pili ya njano, kadi ya pili akiipata baada ya kumchezea rafu Stephane Sessegnon.
    Ataukosa mchezo wa Raundi ya Tano ya Kombe la FA dhidi ya Blackburn Jumamosi.
    Pamoja na yote, bado waliweza kuibuka na ushindi wa 1-0 kwenye Uwanja wa Stadium of Light bao pekee la Santi Cazorla kipindi cha kwanza.
    Fighting: Wilshere and N'Diaye go head to head for the ball
    Wilshere na N'Diaye wakigombea mpira
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: ARSENAL YASHINDA IKIPATA PIGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top