|
MSHAMBULIAJI Zlatan Ibrahimovic alianzia benchi, lakini bado alifunga bao lake la 21 na kuiwezesha timu yake, Paris St Germain kupaa kileleni kwa tofauti wa pointi sita zaidi kufuatia ushindi wa 3-1 nyumbani dhidi ya Bastia jana.
Mshambuliaji huyo wa Sweden, ambaye alichukua nafasi ya Kevin Gameiro dakika ya 65, alifunga kwa penalti likiwa bao la pili, baada ya Jeremy Menez kufunga la kwanza na Ezequiel Lavezzi akafunga la tatu baadaye dakika moja kabla ya mchezo kumalizika, PSG sasa ikifikisha pointi 51 baada ya kucheza mechi 24.Kipa Salvatore Sirigu alishindwa kudaka mechi ya tisa bila kufungwa katika Ligue 1, baada ya kutunguliwa na Wahbi Khazri akiipatia bao la kufutia machozi Bastia, kwa shuti la umbali wa mita 35 la mpira wa adhabu.