KAMARI inalipa. Baada ya miaka kutumia fedha kibao, kusota, vilio hadi kufika Mahakama Kuu, hatimaye Cardiff City ikiongozwa na mkongwe Craig Bellamy imefanikiwa kurejea matawi ya juu baada ya miaka 51 ya kupotea kwenye soka ya England.
Ilikuwa ni sare ya bila kufungana jana dhidi ya Charlotn iliyowahakikishia kupanda Ligi Kuu, jambo ambalo kwa miaka ya karibuni hawakuonekana kuliweza.
Lakini kama ulikuwa una msimu kama waliokuwa nao Cardiff, inawezekana ukasamehewa.
Shangwe: Wachezaji wa Cardiff wakishangilia katika chumba cha kubadilishia nguo baada ya kupanda Ligi Kuu
Mchezaji wa 12 uwanjani: Mashabiki wa Cardiff wakishangilia kurejea Ligi Kuu
Mvinyo wa furaha: Craig Bellamy akigonga shampeni kwenye chumba cha kubadilishia nguo
VIKOSI VYA JANA
Cardiff: Marshall, McNaughton, Turner, Barnett, Taylor, Noone (Smith 71), Kim, Gunnarsson, Mutch, Bellamy, Gestede.
Benchi: Lewis, Whittingham, Cowie, Conway, Mason, Nugent.
Charlton: Hamer, Solly, Morrison, Dervite, Wiggins, Harriott, Hughes (Gower 81), Jackson, Pritchard (Green 88), Kermorgant, Fuller (Obika 81).
Benchi: Button, Taylor, Kerkar, Wilson.
Njano: Fuller.
Njano: Fuller.
Mahudhurio: 26,338
Refa: Scott Mathieson
Cardiff imepanda Ligi Kuu England
Timu hiyo imepanda baada ya kucheza mechi 43 na kufikisha pointi 84 ikiwa kileleni mwa Ligi hiyo, mbele ya Hull City yenye pointi 77, Watford 71 na Brighton & Hove Albion yenye pointi 66.
Ilikuwa ni furaha kubwa jana kwa uongozi, wachezaji na mashabiki wa timu hiyo baada ya sare hiyo ambayo moja kwa moja inawapa tiekti ya kuingia kwenye vita na vigogo msimu ujao katika Ligi Kuu England.
Hawatamsahau refa Scott Mathieson aliyechezesha mechi hiyo iliyowarejesha Ligi Kuu jana mbele ya mashabiki 26, 338.
Cardiff sasa inawaachia vita ya kuwania nafasi nyingine za kupanda Hull City na Watford.