• HABARI MPYA

    Tuesday, April 16, 2013

    KOCHA YANGA AWAPIGA CHABO MAPEMAAAA JKT RUVU WAKILAZIMISHWA SARE NA COASTAL MKWAKWANI LEO

    Beki wa JKT Ruvu, kulia akibutua mpira mbele ya kiungo wa Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga jioni ya leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.

    Kipa wa JKT Ruvu, Shaaban Dihile akidaka mpira wa juu

    Kocha wa makipa wa Coastal, Juma Pondamali kushoto akifurahi na mshambuliaji wa JKT Ruvu, Mussa Hassan Mgosi baada ya mechi

    Hatari kwenye lango la JKT..Beki amelala kupiga kichwa cha mkizi kuokoa

    Mussa Mgosi akipiga kichwa huku kipa wa Coastal, Shaaban Kado akipeleka mikono kuokoa

    Mussa Mgosi akifumua shuti

    Hoi; Mwenyekiti wa Coastal, Ally Aurora akiwa ameshika mashavu yake kwa masikitiko wakati mchezo ukiendelea

    Atupele Green wa Coastal akijaribu kutuliza mpira gambani mbele ya beki wa JKT Ruvu

    Beki wa JKT Ruvu akigombea mpira na kiungo wa Coastal, Suleiman Kassim 'Selembe'

    Wachezaji wa JKT Ruvu wakitoka uwanjani baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza

    Wachezaji wa Coastal wakienda kupumzika...

    Chabo; Kocha wa Yanga, Mholanzi Ernie Brandts katikati akiwa na Msaidizi wake, Freddy Felix Minziro wakifuatilia mechi hiyo, kulia Daktari wa Yanga, Nassor Matuzya. Yanga kesho itamenyana na JKT Mgambo mjini hapa na baada ya hapo itacheza na JKT Ruvu Dar es Salaam

    Jua yako; Mashabiki wa Coastal we acha tu, yaani leo wangeshinda...

    Mashabiki wa Coastal wakifuarahia moja ya kosakosa langoni mwa JKT Ruvu

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: KOCHA YANGA AWAPIGA CHABO MAPEMAAAA JKT RUVU WAKILAZIMISHWA SARE NA COASTAL MKWAKWANI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top