Na Mwandishi Wetu, IMEWEKWA JULAI 17, 2013 SAA 9:15 ALASIRI
AZAM FC imesema kiungo Abdulhalim Humud ‘Gaucho’ si mali yao kwao kwa sasa na wala haihusiki naye kwa lolote, kwa kuwa ilikwishamhamishia Jomo Cosmos ya Afrika Kusini.
Meneja wa Azam FC, Jemadari Said Kazumari ameshangazwa na Humud kuzungumza kwenye kituo cha Redio jana kwamba, Azam inamfanyia kitu kibaya, wakati ni klabu hiyo ndiyo iliyomsaidia kupata timu Afrika Kusini.
“Humud alikwenda Afrika Kusini kufanya majaribio Jomo Cosmos. Wakati anakwenda ilikuwa ajilipie tiketi na akifaulu atarudishiwa fedha zake za tiketi. Bahati nzuri, akafaulu, tena vizuri sana na tunaamini alirudishiwa fedha zake,”.
“Sasa, sisi (Azam) kwa kuwa tulimlipia tiketi ya kwenda Afrika Kusini, tukamkata zile fedha katika mshahara wake. Kilichofuata, sisi tukamalizana na Jomo kwa kuwapa huyo mchezaji, tena bila kuchukua hata senti, kwa makubaliano tu kwamba, wakimuuza, tutapata asilimia 50 ya mgawo,”alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa Kariakoo United ya Lindi.
Jemadari alisema kwamba Humud ameingia Mkataba mnono na Cosmos akipewa mshahara wa dola za Kimarekani 2,000 kwa mwezi, ambayo yote imetokana na juhudi za Azam.
“Sasa anaposema haelewi kinachoendelea kuhusu mustakabali wake sisi tunashindwa kumuelewa, wakati yeye ana Mkataba na Cosmos. Na wakati tunampeleka kule, sisi tulimuambia kabisa, ukikwama rudi hapa (Azam) una haki zote,”.
“Hivyo kama kuna lolote limetokea analoona haliko sawa, alipaswa kuja ofisini kutueleza tujue namna ya kumsaidia, badala ya kwenda kuzungumza utumbo kwenye vyombo vya Habari,”aliongeza Jemadari.
Amesema msimamo wa Azam kwa sasa ni kutolizungumzia kwa undani suala hilo, kwa sababu haielewei chochote hadi hapo itakapokutana na Humud mwenyewe na kupata pia maelezo ya Cosmos.
“Lakini pia kama aliona muda wa kurudi kule umefika na hajatumiwa tiketi, basi angekuja kufanya mazoezi na timu huku (Azam) akisubiri kutumiwa tiketi aende. Maana yake ligi ya Afrika Kusini inaanza Septemba na pengine Cosmos kwa kuwa hawajaanza mazoezi, ndiyo maana hawajamtumia tiketi,”.
“Umefika wakati Humud lazima abadilike sasa na awe na akili za kiutu uzima, vinginevyo pamoja na kuwa mchezaji mzuri hawezi kufanikiwa kwa mambo ya kitoto kama haya,”.
“Ni mtu ambaye amelelewa vizuri sana Azam, karibu makocha wote huwa wanashindwana na tabia zake, lakini uongozi umeendelea kuwa upande wake na hadi mara ya mwisho alipotofautiana na Stewart (Hall) tukaamua kumtafutia timu Afrika Kusini,”aliongeza.

![]() |
Amezomoka; Abdulhalim Humud ameikera Azam FC |