IMEWEKWA JULAI 17, 2013 SAA 7:13 MCHANA
KLABU ya Manchester United imekataa ofa ya kwanza ya Chelsea kwa ajili ya Wayne Rooney - Pauni Milioni pamoja na mchezaji.
BIN ZUBEIRY inafahamu wachezaji wawili walioambatanishwa katika ofa hiyo United ichagua mmoja ni Mchezaji Bora wa Mwaka, Juan Mata au beki Mbrazil, David Luiz.
United imesema Rooney hauzwi na kocha wa Chelsea, Jose Mourinho sasa lazima aamue kuweka gungu tu la maana la fedha mezani.
Lolote mawazoni mwako? Wayne Rooney akiwasili viwanja vya mazoezi vya Manchester United leo kwa mazoezi
Arsenal pia imetoa ofa ya awali ingawa pia imetoa ofa kwa Luis Suarez na Gonzalo Higuain.Klabu hiyo ya Stamford Bridge imeonywa, isithubutu kurejea na ofa ya pili, kwani United haina mpango wa kumuuza Rooney kwa klabu nyingine ya Ligi Kuu England.
Mourinho yu tayari kuwauza Mata na Luiz, ili fedha atakazopata kutokana na mauzo ya wawili hayo atumie kumnunua mchezaji wa United.
Rooney anafikiri amefikia kilele cha mustakabali wake na hana zaidi cha kuthibitisha baada ya misimu tisa Old Trafford.
Inafahamika mshambuliaji huyo wa England amechanganyikiwa na kukerwa na maneno ya kocha mpya, David Moyes kwamba hatauzwa sababu ndiye mbadala wa mshambuliaji chaguo la kwanza, Robin van Persie.
Chelsea imewaofa United Juan Mata (juu) au David Luiz (chini) pamoja na Pauni Milioni 10 wapewe Rooney
Mourinho aliwasha moto jana katika jitihada zake za kuwania saini ya Rooney kwa kutoa onyo kwamba, matumaini ya England yatakuwa madogo Kombe la Dunia kama mchezaji huyo atabakia United.
Chelsea imehamishia nguvu zake kwa Rooney baada ya wachezaji iliyokuwa inawataka awali kuwakosa wote, Radamel Falcao amekwenda Monaco na Edinson Cavani katua PSG, zote za Ufaransa.
Chelsea imehamishia nguvu zake kwa Rooney baada ya wachezaji iliyokuwa inawataka awali kuwakosa wote, Radamel Falcao amekwenda Monaco na Edinson Cavani katua PSG, zote za Ufaransa.
Mourinho alisema: "Ikiwa Wayne ni chaguo la pili kwa Manchester United, kisha timu ya taifa itaathirika.’
HII NDIYO SABABU CHELSEA INAWATOA JUAN MATA AU DAVID LUIZ?
Umri: Miaka 25
Nafasi: Kiungo mshambuliaji
Klabu za awali: Real Madrid B, Valencia
Takwimu za Chelsea:
2011-12: Mechi: 54 Mabao: 12 Pasi za mabao: 23
2012-13: Mechi 64 Mabao 20 Pasi za mabao 35
Hispania: Mechi: 29 Mabao 8.
VIDEO: Mabao matamu ya Juan Mata Chelsea
Umri: Miaka 26
Nafasi: Beki/Kiungo
Klabu za awali: Vitoria, Benfica
Takwimu za Chelsea:
2010-11: Mechi:12 Mabao: 2
2011-12: Mechi 40 Mabao 3
2012-13: Mechi 57 Mabao 7
Brazil: Mechi 28 Hajafunga.
VIDEO: Bao tamu la David Luiz dhidi ya Basle katika Europa League