• HABARI MPYA

    Friday, July 05, 2013

    FAINALI AIRTEL RISING STARS ‘LIVE’ SUPERPORT

    Na Boniface Wambura, IMEWEKWA JULAI 5, 2013 SAA 11:20 JONI
    FAINALI za michuano ya Airtel Rising Stars kwa wavulana na wasichana zinazochezwa kesho (Julai 6 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam zitaoneshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha SuperSport.
    Vijana katika michuano ya Airtel Rising Stars

    Mechi za fainali ambazo mgeni rasmi atakuwa Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala zitachezwa kuanzia saa 7.30 mchana kwa wasichana wakati ile ya wavulana itaanza saa 9.30 alasiri.
    Nusu fainali za mashindano hayo ambazo pia zinaonekana moja kwa moja SuperSport zinachezwa leo (Julai 5 mwaka huu). Kwa upande wa wasichana ni kati ya timu za Kinondoni na Kigoma wakati Ilala inaumana na Temeke.
    Kwa upande wa wavulana nusu fainali ya kwanza ni kati ya Mwanza na Ilala ambapo baadaye itafuatiwa na nyingine kati ya Morogoro na Kinondoni. Mechi za kutafuta mshindi wa tatu zitachezwa kesho asubuhi (Julai 6 mwaka huu).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: FAINALI AIRTEL RISING STARS ‘LIVE’ SUPERPORT Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top