Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA JULAI 14, 2013 SAA 3:06 ASUBUHI
WINGA aliyeichachafya ngome ya Tanzania katika mchezo wa jana dhidi ya Uganda, kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), Brian Majwega amesema yupo tayari kusaini moja ya timu tatu kubwa za hapa, Azam FC, Simba na Yanga SC zikimtangazia dau la maana.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana katika hoteli ya Sapphire Court, Dar es Salaam, Majwega aliyetoa krosi ya bao pekee la ushindi la Uganda lililofungwa na Dennis Iguma dakika ya 46 alisema anakaribisha ofa.
“Hakuna tatizo, timu yoyote ikinihitaji na ije tu, hapa Tanzania ni sawa na nyumbani tu, ndugu zangu wamecheza na wanacheza hapa. Na mimi naamini naweza kupata mafanikio zaidi nikija hapa,”alisema.
Mshambuliaji huyo wa mabingwa wa Uganda, KCC ya Kampala, alikuwa kivutio katika mchezo wa jana akiwachachafya kwa chenga maridadi na kasi yake wachezaji wa Stars na kwa kiasi kikubwa alikuwa kila kitu kwenye ushindi wa jana wa Uganda.
Pamoja na Majwega kuwaita Azam, Simba na Yanga, lakini kocha wake, Milutin Sredojevich ‘Micho’ ameonya. “Waambie wasithubutu kumsogelea mchezaji wangu yoyote kwa sasa, hadi baada ya mechi ya marudiano, tena wakitaka waje kuchukua timu nzima,”alisema.
Baada ya mechi ya jana, Uganda ikishinda 1-0 sasa inatakiwa hata sare katika mchezo wa marudiano nyumbani wiki mbili zijazo ili ikate tiketi ya kwenda Afrika Kusini kwenye CHAN.

![]() |
Kutoka kulia Micho, Majwega na Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwanaspoti, Frank Sanga jana Sapphire Court Hotel |