IMEWEKWA AGOSTI 6, 2013 SAA 1:37 ASUBUHI
KAMA Arsene Wenger alihitaji ukumbusho wowote wa kosa alilofanya katika usajili akiwa kazini Arsenal, Didier Drogba alifanya hivyo Uwanja wa Emirates Jumapili.
Mabao mawili ya Drogba ya dakika za lala salama dhidi ya Arsenal yaliyowezesha Galatasaray kubeba Kombe la Emirates yameendeleza rekodi ya mshambuliaji huyo dhidi ya The Gunners na kufika mabao 15 katika mechi 15.
Kwamba, katika dakika 1175 ambazo Drogba amecheza dhidi ya Arsenal, amefunga wastani wa bao moja katika kila dakika 78 na sekunde 20.
Alifunga: Mabao mawili ya dakika za lala salama ya Drogba aliyoifungia Galatasaray ikibeba Kombe la Emirates yameendeleza rekodi yake ya kuwafunga Arsenal
REKODI YA MABAO YA DROGBA LIGI KUU DHIDI YA TOP FIVE
WAPINZANI | MABAO | MECHI ALIZOCHEZA | MABAO KWA MECHI |
Arsenal | 8 | 11 | 0.73 |
Man City | 5 | 13 | 0.38 |
Spurs | 3 | 14 | 0.21 |
Liverpool | 2 | 12 | 0.17 |
Man Utd | 1 | 11 | 0.09 |
Ulikuwa usiku wa pigo kwa Wenger, ambaye alikataa kumsajili Drogba kwa Pauni 100,000.
Akiwa anachipukia nyota huyo wa Ivory Coast katika miaka yake minne Le Mans kati ya mwaka 1998 na 2002, jicho la skauti wa Wenger lilimnasa mchezaji huyo.
Wenger alikataa kumsajili, na Drogba akahamia timu nyingine ya Ligue 1, Guingamp akiwa ana umri wa miaka 23 kwa Pauni 80,000.
Wenger alisema mwaka 2009: "Tumemuangalia kwa umakini alipokuwa Le Mans. Siyo sisi tu tuliomuangalia. Lakini tulifikiri hawezi tayari kiasi cha kutosha.
"Lilikuwa ni kosa, lakini ukiwa kwenye soka, kila mmoja anaweza kuelewa. Tulikuwa na Thierry Henry. Tulisema tutafuatilia maendeleo ya Drogba. Hatukuwahi kumkataa,".
Maumivu zaidi: Wenger aliachiwa pigo na Drogba alipoisambaratisha Arsenal yake Jumapili
UMUHIMU WA DROGBA
Katika mechi 35 zilizopita za Ligi Kuu kati ya Arsenal na Chelsea, rekodi ya The Blues ikiwa na Drogba ni nzuri mno tofauti waakti hayupo.Akiwepo: W7 D3 L1 Hayupo: W2 D9 L13
Mwaka 2004, kufuatia msimu wa mafanikio makubwa akiwa Marseille, Drogba alisaini Chelsea kwa ada ya Pauni Milioni 24.
Kana kwamba hilo halikuwa pigo tosha katika jino la Wenger, Drogba aliifanyizia ile mbaya timu yake uwanjani.
Alifunga mabao 13 katika mechi 14 dhidi ya Arsenal enzi zake akiwa Stamford Bridge, mengi kati yao akifunga katika mechi muhimu.
Wenger alipata ahueni wakati Drogba alipoondoka Chelsea kuhamia Shanghai Shenhua mwaka jana, akisema wakati huo: "Sijui ni kiasi gani Chelsea wamempoteza, lakini hatumkumbuki. Amefanya madhara mengi dhidi yetu katika kila mechi,".
Drogba anaweza kuwa ukingoni mwa soka yake akiwa na umri wa miaka 35 sasa, lakini kwa Emirates atabakia kukumbukwa kama kiboko ya timu ya Wenger hadi siku atakapotungika daluga zake.
Mfaransa huyo sasa atakuwa anaomba dua Arsenal isipagwe kundi moja na Galatasaray katika Ligi ya Mabingwa katika droo inayotarajiwa kupangwa mjini Monaco Agosti 29.
BIN ZUBEIRY INAKULETEA PICHA KUTOKA MECHI 15 ZA DROGBA DHIDI YA ARSENAL...
Agosti 7, 2005 - Ngao ya Jamii- Chelsea 2-1 Arsenal
Drogba alifungua akaunti yake ya mabao dhidi ya Arsenal mwaka 2005 katika Ngao ya Jamii Uwanja wa Millennium, Cardiff, akifunga dakika ya nane
Drogba aliifungia bao la pili katika ushindi wa 2-0 kwa Chelsea dakika ya 58
Agosti 21, 2005 - Ligi Kuu - Chelsea 1-0 Arsenal
Drogba alifunga bao la kubahatisha na kuipa ushindi wa kwanza Chelsea katika Ligi Kuu dhidi ya Arsenal ndani ya miaka karibu 10
Februari 25, 2007 - Fainali ya Carling- Chelsea 2-1 Arsenal
Baada ya Theo Walcott kufunga la kwanza dakika ya 12 Uwanja wa Millennium, Drogba alisawazisha dakika nane baadaye
Drogba alifunga la ushindi zikiwa zimesalia dakika sita na kubeba Kombe la Carling
Machi 23, 2008 - Ligi Kuu - Chelsea 2-1 Arsenal
Baada ya kuwa nyuma kwa 1-0 Uwanja wa Stamford Bridge, Drogba alisawazisha dakika ya 73 kwa shuti dhaifu
Mabao mengine mawili kwa Drogba, akifunga la ushindi dakika ya 82
Aprili 18, 2009 - Nusu Fainali FA- Arsenal 1-2 Chelsea
Bao la ushindi la Drogba dakika ya 84 Uwanja wa Wembley liliipeleka Chelsea fainali
Novemba 29, 2009 - Ligi Kuu - Arsenal 0-3 Chelsea
Drogba aliwafungia wageni bao la kwanza dakika ya 41 akiunganisha krosi ya Ashley Cole
Drogba alihitimisha ushindi wa 3-0 Uwanja wa Emirates kwa shiti la mita 25 la mpira wa adhabu baadaye
Februari 7, 2010 - Ligi Kuu - Chelsea 2-0 Arsenal
Katika mechi ambayo Arsenal ilitakiwa kushinda kuweka hai matumaini ya ubingwa, Drogba alifunga bao la kwanza dakika ya nane
Drogba akaifungia la pili Chelsea dakika ya 23
Oktoba 3, 2010 - Ligi Kuu - Chelsea 2-0 Arsenal
Krosi ya Ashley Cole karibu na nguzo ya lango ilikutana na Drogba akafunga bao la kwanza dakika ya 39
Agosti 4, 2013 - Kombe la Emirates- Arsenal 1-2 Galatasaray
Zikiwa zimesalia dakika 11 Arsenal kusherehekea Kombe la Emirates, Drogba alisawazisha kwa penalti
Drogba alifunga bao lake la 15 dhidi ya Arsenal na kutwaa Kombe la Emirates akiwa na Galatasaray, baada ya kazi nzuri ya Wesley Sneijder waliyeingia naye kipindi cha pili siku hiyo.