• HABARI MPYA

    Friday, August 09, 2013

    ARSENAL YAPANGIWA KIGONGO LIGI YA MABINGWA, YAPEWA FENERBAHCE NA MECHI NI AGOSTI 20

    IMEWEKWA AGOSTI 9, 2013 SAA 11:36 JIONI
    KLABU ya Arsenal imepangiwa mchezo mgumu wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Fenerbahce ya Uturuki.
    Celtic itacheza na Shakhter Karagandy, ambao wamefika hatua hii kwa mara ya kwanza. 
    Mechi za kwanza zitachezwa Agosti 20 na 21 na marudiano wiki inayofuata. Inamaanisha Arsenal itakuwa mechi nne ndani ya siku 10 wiki mbili zijazo.
    All smiles: Arsenal players Jack Wilshere and Mikel Arteta will face Fenerbahce in the play-offs
    Tabasamu kwa wote: Wachezaji wa Arsenal, Jack Wilshere na Mikel Arteta watamenyana na Fenerbahce katika mechi ya kuwania kucheza Ligi ya Mabingwa
    Fenerbahce wanasubiri uamuzi wa mwisho kutoka Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) kujua kama wataruhusiwa kuendelea na mashindano hayo msimu huu, baada ya kufungiwa kucheza Ulaya na UEFA kwa tuhuma za kupanga matokeo kwenye mashindano ya nchini mwake.
    Wamepinga uamuzi huo na CAS inatarajiwa kuta uamuzi kabla ya kutajwa kwa droo ya hatua ya makundi, lakini mechi za nyumbani na ugenini na Arsenal zitaendelea kabla ya uamuzi kutolewa.
    Old foes: Robin van Persie played last time Arsenal and Fenerbahce met in 2008
    Enzi hizo: Robin van Persie alicheza mara ya mwisho Arsenal ilipokutana na Fenerbahce mwaka 2008

    Arsenal iliipiku Tottenham katika nafasi ya nne msimu uliopita Ligi Kuu England na kupata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa.
    Celtic imefika hatua hiyo baada ya kuing'oa Elfsborg ya Sweden 1-0 katika mechi za kuwania kufuzu kucheza michuano hiyo, shukrani kwake mfungaji wa bao pekee katika mechi zote mbili, Kris Common Uwanja wa Celtic Park.

    HII NDIYO FENERBAHCE...

    Nchi: Uturuki Msimu uliopita: Nafasi ya pili Ligi Kuu 
    Michuano ya Ulaya: Robo Fainali, 2007-2008
    Uwanja na ukubwa: Sukru Saracoglu, watu 50,509
    Mafanikio: Ubingwa Ligi ya Uturuki mara 18 (mwisho 2010-2011); Kombe la Uturuki mara sita (mwisho 2012-2013); Super Cup ya Uturuki mara nane (mwisho 2009)
    Kocha: Ersun Yanal – Alianza kujulikana akiwa Genclerbirligi ilipozitoa Blackburn Rovers, Parma na Sporting Lisbon Kombe la UEFA msimu wa 2003-2004. Amewahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya Uturuki kati ya 2004 na 2005, akiiweka katika nafasi ya kucheza Kombe la Dunia nchini Ujerumani kabla ya kubadilishwa na Fatih Terim.  
    Wachezaji iliyosaini majira haya ya joto: Emmanuel Emenike (Spartak Moscow, Pauni Milioni 11.4); Alper Potuk (Eskisehirspor, Pauni Milioni 6.38); Bruno Alves (Zenit St Petersburg, Pauni Milioni 4.84); Michal Kadlec (Bayer Leverkusen, Pauni Milioni 3.96) 
    Nahodha: Emre Belozoglu – Mashabiki wa Newcastle United watakuwa wanamkumbuka huyu jamaa ambaye alicheza kwa miaka mitatu St James’ Park kati 2005 na 2008, zaidi kutokana na kufunga bao la ushindi kwa mpira wa adhabu dhidi ya Sunderland. 
    Mtu wao hatari: Moussa Sow – Mshambuliaji wa Senegal ambaye ameiongoza kwa mafanikio Fenerbahce tangu ajiunge nayo akitokea Lille kwa Pauni Milioni 8, Januari 2012, akifunga mabao 22 katika mechi 42 alizocheza tangu awasili. 
    Mechi zilizopita: 
    Kombe la Washindi la UEFA, Raundi ya kwanza 1979-1980 – Arsenal 2 (Alan Sunderland, Willie Young) Fenerbahce 0 na Fenerbahce 0 Arsenal 0
    Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi 2008-2009 – Fenerbahce 2 Arsenal 5 (Emmanuel Adebayor, Theo Walcott, Abou Diaby, Alexander Song, Aaron Ramsey) na Arsenal 0 Fenerbahce 0. 

    DROO YA KUWANIA KUCHEZA HATUA YA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA UALAYA...

    Dinamo Zagreb (Croatia) v Austria Vienna  (Austria)
    Ludogorets Razgrad (Bulgaria) v FC Basle
    Viktoria Pilzen (Jamhuri ya Czech) v NK Maribor (Slovenia)
    Shakhter Karagandy (Kazakhstan) v Celtic (Scotland)
    Steaua Bucharest (Romania) v Legia Warsaw (Poland)
    Lyon (Ufaransa) v Real Sociedad (Hispania)
    Schalke (Ujerumani) v Metalist Kharkiv (Ukraine)
    Pacos de Ferreira (Ureno) v Zenit St Petersburg (Urusi)
    PSV Eindhoven (Uholanzi) v AC Milan (Italia)
    Fenerbahce (Uturuki) v Arsenal (England)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: ARSENAL YAPANGIWA KIGONGO LIGI YA MABINGWA, YAPEWA FENERBAHCE NA MECHI NI AGOSTI 20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top