• HABARI MPYA

    Friday, August 09, 2013

    KUMEKUCHA SIMBA SC KESHO TAIFA, SIMBA KWELI HAWEZI KUKOSA

    Na Ezekiel Kamwaga, IMEWEKWA AGOSTI 9, 2013 SAA 12:20 JIONI
    SIMBA SC kesho inatarajiwa kuazimisha kile kinachoitwa Siku ya Simba (SIMBA DAY) katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
    Utaratibu wa kuwa na Simba Day ulianzishwa na klabu kwa lengo la kuwa na siku ambapo wapenzi, wanachama, viongozi, wachezaji wa zamani na wa sasa pamoja na watu wengine mashuhuri, hukutana kwa pamoja na kusherehekea klabu ambayo imewafanya wawe wamoja pamoja na tofauti nyingi walizonazo.
    Simba SC

    Mwaka huu, shughuli hiyo itafanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine, Simba SC inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki na klabu ya soka ya Sports Club Villa kutoka nchini Uganda.
    Katika kusherehesha tukio hilo, wasanii maarufu kama vile Juma Nature, Tunda Man na Snura maarufu kwa jina la ‘Mama Majanga’ watatumbuiza uwanjani hapo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: KUMEKUCHA SIMBA SC KESHO TAIFA, SIMBA KWELI HAWEZI KUKOSA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top