IMEWEKWA AGOSTI 9, 2013 SAA 4:15 USIKU
KLABU ya Tottenham imekamilisha uhamisho wa kiungo wa Toulouse, Etienne Capoue wa Pauni Milioni 8.6 baada ya vipimo vya afya.
Ada ya uhamisho wa mwasoka huyo wa kimataifa wa Ufaransa, ambaye pia alikuwa anatakiwa na Cardiff City na Atletico Madrid, unahusisha na malipo mengine.
Capoue, mwenye umri wa miaka 24, ni kiungo mkabaji, lakini mchezaji huyo mwenye urefu wa futi 6 na inchi 2, anaweza kucheza kama beki wa kati.
Usajili mpya wa AVB: Etienne Capoue amejiunga na Tottenham kutoka Toulouse
Tottenham inahitaji kujiimarisha baada ya kumuuza Steven Caulker na ikiwa na inakabiliwa na tatizo la majeruhi kwa Jan Vertonghen na Younes Kaboul.
Capoue, ambaye amefunga mabao saba katika mechi 34 za ligi msimu uliopita, aliingia kwenye hesabu za Andre Villas-Boas tangu January na Mreno huyo amtimiza ndoto zake kumnasa.
Tottenham bado inamuwania kiungo wa Roma, Miralem Pjanic, mwenye umri wa miaka 23, wakati majadiliano ya kuimarisha zaidi kikosi yanaendelea, akiwemo winga Jese Rodriguez, kuhusishwa katika biashara na Real Madrid juu ya Gareth Bale.
Capoue, kushoto, anaonekana hapa akipambana na mchezaji wa Bordeaux, Henri Saivet, amesaini Spurs