IMEWEKWA AGOSTI 9, 2013 SAA 4:43 USIKU
KOCHA Arsene Wenger amesema kwamba hajakata tamaa ya kumsaini Luis Suarez licha ya mmiliki wa Liverpool, John Henry kukataa kumuuza mshambuliaji wake huyo kwa Arsenal.
Ofa ya The Gunners ya Pauni Milioni 40 kwa imepigwa chini kwa Suarez – ambaye amelazimishwa kufanya mazoezi peke yake kutokana na kulazimisha kuondoka, huku Liverpool ikikana kusaini naye Mkataba wa kumruhusu kuondoka.
Wenger alikutana na maswali kuhusu suala hilo wakati Arsenal ilipotua Helsinki mchana wa leokuelekea mchezo wa kesho wa kirafiki wa kujiandaa na msimu dhidi ya Manchester City.
Utata mtupu: Suala la Luis Suarez kuondoka Liverpool limetawala majira haya ya joto
Alipoulizwa kama kauli ya Henry itamkatisha tamaa katika jitihada za kumsaini Suarez, kocha wa Arsenal alisema: "Hapana, kwa sababu tupo katikati ya uhamisho na tunaangalia uwezekano wa kuimarisha kikosi.
"Sijasoma taarifa yake, lakini ni kwamba inaweza kufanikiwa au hapana. Tutaendelea kuwa na matumaini pamoja na ambavyo anafanya. Sina cha kuongeza zaidi ya nilichosema kuhusu uhamisho wa Suarez. Itafanikiwa, itafanikiwa katika njia za heshima na Liverpool,"alisema.
Bwana Profesa: Wenger yupo Helsinki na timu yake kwa mechi ya kujiandaa na msimu
Wachezaji wa Arsenal wakiwasili Helsinki
Arsene Wenger kulia akiwa na Aaron Ramsey leo wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari
Kikosi cha Wenger bado ni miongoni mwa vikosi vinavyotarajiwa kufanya vizuri Ligi Kuu England