IMEWEKWA AGOSTI 8, 2013 SAA 7:48 MCHANA
KLABU ya Barcelona haijapoteza muda katika kuwania saini ya Daniel Agger, baada ya kuonywa kuhusu David Luiz, na imetoa ofa ya Pauni Milioni 17 kumtaka beki huyo wa Liverpool.
Chelsea iliwaka baada ya ofa ya awali ya Pauni Milioni 34.5 kwa ajili ya Luiz kwa kuipiga chini na kuwaambia Barcelona wasijisumbue kurejea tena na ofa yoyote, kwani beki wao Mbrazil hauzwi kwa bei yoyote.
Anayetakiwa: Agger anatakiwa na vigogo wa Hispania, Barcelona baada ya kumkosa Luiz
Ujumbe unaonekana kufika nyumbani na vyanzo nchini Denmark vimesema leo kwamba vigogo wa Nou Camp wameanza harakati za kumsajili Agger na wametoa ofa ya Pauni Milioni 17 mezani kumuondoa Anfield.
Hii inaleta wakati mwingine mgumu kwa kocha Brendan Rodgers, ambaye yupo katikati ya sakata la Luis Suarez, kutokanana Agger kutakiwa na Barcelona, lakini mabosi wa Anfield wamesema hawana mpango wa kuuza mchezaji wao yeyote.
Wamebadili malengo: Agger sasa anatakiwa na vigogo wa Katalunya baada ya ofa yao ya kumtaka Luiz kutupwa kapuni na Chelsea