• HABARI MPYA

    Friday, August 02, 2013

    KIIZA AREJEA DAR LEO KWA MARA YA TANO KWA AJILI YA KUSAINI YANGA

    Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA AGOSTI 2, 2013 SAA 2:38 USIKU
    HII sasa inaweza kuwa sehemu ya mwsiho ya filamu ya Yanga SC na Hamisi Friday Kiiza ‘Diego’. Mshambuliaji huyo wa Uganda ametua Dar es Salaam jioni ya leo kwa ajili ya kuja kusaini Mkataba wa kuendelea kuichezea klabu hiyo baada ya zoezi hilo kushindikana mara nne awali.
    Kiiza ametua Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam majira ya Saa 12 jioni na kati ya leo usiku na kesho mchana atakuwa amekwishamalizana na Yanga.
    Amerudi tena; Hamisi Kiiza amerejea tena leo kwa mara ya tano kwa ajili ya kusaini Yanga SC

    Hii ni mara ya tano, Kiiza anakuja Dar es Salaam kwa ajili ya suala la kusaini Mkataba na mara nne zote za awali, alishindwa kuafikiana na uongozi wa klabu hiyo akarejea Uganda, mara ya mwisho ikiwa ni wiki iliyopita.
    Awali, mara tu baada ya Ligi Kuu, Yanga ilifanya mazungumzo na mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda, hawakufikika makubaliano akaondoka. Mara ya pili, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Mussa Katabaro akapanda ndege Uganda kuzungumza naye, wakafikia makubaliano akamtumia tiketi aende Dar es Salaam.
    Hata hivyo, mpachika mabao huyo alipofika Dar es Salaam akaona kama anapotezewa muda, kwa sababu Yanga ilionekana kutegeshea matokeo ya majaribio ya mshambuliaji kutoka Nigeria, Ogbu Brendan Chukwudi, akifuzu imteme Kiiza, na Mganda huyo akapanda ndege kurejea Kampala.
    Yanga SC baada ya kugundua Chukwudi ni majeruhi wa muda mrefu, ikamtumia tiketi Kiiza mwishoni mwa mwezi uliopita arejee tena Dar es Salaam, lakini pia akapanda ndege kurejea Uganda, bila kusaini Mkataba.
    Tayari mshambuliaji Mnigeria, Ogbu Brendan Chukwudi amerejeshwa kwao baada ya kuonekana ni majeruhi sugu.
    Akisaini, Kiiza atakuwa mchezaji wa nne katika orodha ya wachezaji wa kigeni baada ya beki Mbuyu Twite, kiungo Haruna Niyonzima wote kutoka Rwanda na mshambuliaji Didier Kavumbangu wa Burundi, hivyo klabu itabakiza nafasi moja.
    Wakati huo huo, Yanga inapambana na Simba SC kuwania saini ya Mganda mwingine, Moses Oloya ambaye anamaliza Mkataba wake na Saigon Xuan Thanh ya Vietnam mwezi huu, Agosti.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: KIIZA AREJEA DAR LEO KWA MARA YA TANO KWA AJILI YA KUSAINI YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top