• HABARI MPYA

    Friday, August 02, 2013

    SCHMEICHEL AMPIGIA KING'ORA IBRAHIMOVIC MAN UNITED, ASEMA ATAKUWA CANTONA MWINGINE OLD TRAFFORD

    IMEWEKWA AGOSTI 2, 2013 SAA 1:10 JIONI
    KIPA wa zamani na gwiji wa klabu ya Manchester United, Peter Schmeichel anaamini Zlatan Ibrahimovic alizaliwa kwa ajili ya kuchezea Mashetani hao Wekundu na atapenda kumuona anachezea klabu hiyo.
    Amesema mshambuliaji huyo wa Paris Saint-Germain atakuwa kama gwiji wa zamani wa United, Eric Cantona na kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 atakuwa kipenzi cha mashabiki.
    Future Red Devil? Zlatan Ibrahimovic is a current first team star at Paris-Saint Germain
    Shetani Mwekundu baadaye? Zlatan Ibrahimovic kwa sasa ni nyota wa kikosi cha kwanza Paris-Saint Germain
    Cantona alitua Old Trafford akitokea Leeds kwa dau la Pauni Milioni 1.2, Novemba mwaka 1992 na mwishoni mwa msimu wake wa kwanza alikuwa chachu ya klabu hiyo kutwaa taji lake la kwanza la Ligi Kuu baada ya miaka 26, kabla ya kuifanya United itawale zaidi soka ya nchi hiyo.
    Schmeichel ameliambia gazeti la Sweden, Expressen kwamba: "Umewahi kumuuliza Zlatan kwa nini hajacheza England bado, lakini ningependa kummuona anacheza Manchester United.
    "Sijui anamshabikia nani, lakini amezaliwa kuwa mchezaji wa Manchester United, wazi atang'ara. Nafikiri mashabiki wetu watampenda, kama hatahamia, hatahamia tena. Kwa Zlatan kucheza namna tunavyopenda acheze, atakuwa Zlatan. 
    New era: Eric Cantona (left) and Peter Schmeichel pose with the FA Cup after beating Liverpool in the 1996 final
    Zama mpya: Eric Cantona (kushoto) na Peter Schmeichel wakiwa na Kombe la FA baada ya kuifunga Liverpool katika fainali mwaka 1996
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: SCHMEICHEL AMPIGIA KING'ORA IBRAHIMOVIC MAN UNITED, ASEMA ATAKUWA CANTONA MWINGINE OLD TRAFFORD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top