IMEWEKWA AGOSTI 2, 2013 SAA 12:55 JIONI
KLABU ya Newcastle inajiandaa kukamilisha usajili wao wa kwanza mwishoni mwa dirisha baada ya kukubali kumsajili mshambuliaji wa Lyon, Bafetimbi Gomis.
Uhamisho wa Gomis kutua The Magpies utakamailishwa na Mkurugenzi wa Sika, Joe Kinnear, huku dili likiwa katika mwelekeo wa kufanikiwa kwa mujibu wa Rais wa klabu hiyo ya Ufaransa, Jean-Michel Aulas.
Newcastle italipa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 8.7 kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, ambaye alifunga mabao 16 Lyon msimu uliopita, Aulas aliliambia gazeti Le Journal du Dimanche la Ufaransa.
Mtu wa kwanza ndani: Mshambuliaji wa Lyon, Bafetimbi Gomis yuko njiani kutua Newcastle
Habadiliki: Gomis anatarajiwa kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha wa Toon, Alan Pardew majira haya ya joto


.png)