• HABARI MPYA

    Friday, August 02, 2013

    MSIBA COASTAL UNION, IDRISA NGULUNGU AFARIKI DUNIA

    Na Saidy Mdoe, IMEWEKWA AGOSTI 2, 2013 SAA 12:49 JIONI
    MCHEZAJI wa zamani wa Coastal Union ya Tanga, Idrisa Ngulungu amefariki dunia mapema leo.
    Idirisa Ngulungu alitamba na Costal Union mwishoni mwa miaka ya themanini hadi mwanzoni mwa miaka ya tisini.
    Alikuwepo kwenye kikosi kilichotwaa ubingwa wa Tanzania Bara mwaka 1988.
    Kwa mujibu wa kaka wa marehemu, Hussein Ngulungu ambaye nae ni mchezaji wa zamani wa Taifa Stars amesema Idrisa amefariki kwa ajali ya gari iliyotokea eneo la Kisaki mkoani Morogoro.
    Idrisa Ngulungu (kushoto) enzi za uhai wake. Hapa alikuwa amemtembea Mkurugenzi wa Ufundi wa Coastal Union, Alhaj Nassor Mohamed Bin Slum ofisini kwake, Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam mwezi uliopita. 

    Hussein Ngulungu ameiambia Saluti5 kuwa Idrisa na ndugu wengine walikuwa wanaelekea Kisaki kwenye mazishi na kwa bahati mbaya gari walilokuwa wanasafiria lilichomoka tairi la mbele na kusababisha ajali hiyo iliyopoteza maisha ya Idirsa pamoja na ngugu yake mwingine wa kike.
    Hussein Ngulungu amesema bado wanashughulikia kupata mwili wa marehemu na mazishi yanategemewa kufanyika kesho mjini Morogoro mjini. (Habari ni haki ya Saluti5.com)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MSIBA COASTAL UNION, IDRISA NGULUNGU AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top