IMEWEKWA AGOSTI 3, 2013 SAA 10:07 JIONI
KLABU ya Real Madrid imewapiga bao wapinzani wao, Barcelona katika harakati za kumgombea kinda mwenye umri wa miaka 11, Mmarekani Joshua Pynadath.
KLABU ya Real Madrid imewapiga bao wapinzani wao, Barcelona katika harakati za kumgombea kinda mwenye umri wa miaka 11, Mmarekani Joshua Pynadath.
Nyota huyo chipukizi alifanya na timu zote hizo kabla ya kuamua kwenda Madrid.
Wameingia Mkataba wa mwaka mmoja na msambuliaji huyo kinda mwenye kipaji kujiunga na akademi yao.
Pichani: Kinda mwenye kipaji, Joshua Pynadath amesaini Real Madrid
Pynadath anakuwa Mmarekani wa kwanza kujiunga na mfumo wa soka ya vijana wa Madrid, ambao umezalisha wakali kama magiwji wa Los Blancos, Iker Casillas, Raul na Guti.
Madrid ilipewa taarifa za kipaji cha kinda huyo na Jeff Baicher, Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya sasa ya Pynadath, De Anza Force Soccer Club.
Baicher aliwapeleeka viongozi wa Real video ya vipande vya michezo ya kinda huyo akionyesha uwezo wa kumiliki mpira, kupiga chenga, kutoa pasi na kufumua mashuti mwaka uliopita na ilitosha kuwashawishi kumkaribisha kwa majaribio ya wiki moja, mwishoni mwa Novemba.
Mshambuliaji huyo kutoka Los Altos Hills, California, alifanya ya kutosha kujipatia nafasi nyingine ya majaribio mwaka huu na pia kuwavutia vigogo wengine wa Hispania, Barcelona.
Alitumia siku 17 katika akademi ya Barca, iitwayo La Masia lakini baadaye akapewa ofa ya kujiunga na Madrid, Alevin A Team.
Pynadath amefanya mazoezi katika mazingira yale yale wakati Lionel Messi alipokuwa kwa majaribio Barcelona
Shujaa: Joshua ataungana na Cristiano Ronaldo klabu ya Madrid


.png)