Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA AGOSTI 3, 2013 SAA 12:29 JIONI
SIMBA SC imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Kombaini ya Polisi jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mfululizo wa michezo ya kujiandaa na msimu.
Hadi mapumziko, Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililotiwa kimiani na mshambuliaji wa zamani wa Pamba FC ya Mwanza, Betram Mombeki.
Mombeki aliyekuwa akiishi Marekani kwa muda mrefu, alifunga bao hilo kwa shuti zuri akiunganisha krosi ya Sino Augustino dakika ya 17 kutoka wingi ya kushoto.
Safari hii Mombeki hakushangilia kwa staili ya marehemu Rashid Yekini kuingia nyavuni kucheza, bali alikwenda kwa mashabiki na kusherehekea nao.
Mombeki alikaribia kufunga mara mbili kabla ya mapumziko, mara moja akipiga shuti likienda nje sentimita chache na mara nyingine akipiga kichwa kikipaa juu sentimita chache.
Kipindi cha pili, Polisi walibadilika na kuanza kucheza vizuri, wakishambulia kwa kasi nzuri lango la Simba. Kutokana pia na kutoka kwa viungo wawili wazoefu wa Simba SC, Abdulhalim Humud ‘Gaucho’ na Ramadhan Chombo ‘Redondo’, Polisi walifanikiwa kutawala safu ya kiungo.
Kwa sababu hiyo, haikuwa ajabu Nicolas Kabipe alipoisawazishia Polisi dakika ya 60 kufuatia kazi nzuri ya kiungo Bantu Admin, aliyekuwa akiisumbua ngome ya Simba SC leo.
Kufa kwa safu ya kiungo ya Simba SC kulimfanya hata mshambuliaji Mombeki akose watu wa kumtengenezea nafasi za kufunga kipindi cha pili.
Katika mchezo wa leo, kikosi cha Simba SC kilikuwa; Andrew Ntalla, Nassor Masoud ‘Chollo’, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Miraj Adam, Rahim Juma, Jonas Mkude, Said Ndemla, Abdulhalim Humud, Betram Mombeki, Sino Augustino na Ramadhan Chombo ‘Redondo’.
Polisi FC; Kondo Salum, Eliasa Maftah, Simon Fanuel, Yahya Khatib, Salmin Kiss, Salum Nahoda, Magige Machango, Andrew Bundala, Mokili Lambo, Bantu Admin na Nicolas Kapibe.

![]() |
| Mnasemaaa? Naitwa Betram Mombeki Mabao; Betram akishangilia bao lake leo |
Mombeki alikaribia kufunga mara mbili kabla ya mapumziko, mara moja akipiga shuti likienda nje sentimita chache na mara nyingine akipiga kichwa kikipaa juu sentimita chache.
Kipindi cha pili, Polisi walibadilika na kuanza kucheza vizuri, wakishambulia kwa kasi nzuri lango la Simba. Kutokana pia na kutoka kwa viungo wawili wazoefu wa Simba SC, Abdulhalim Humud ‘Gaucho’ na Ramadhan Chombo ‘Redondo’, Polisi walifanikiwa kutawala safu ya kiungo.
![]() |
| Utamu wa bao; Betram akikimbia kushangilia baada ya kufunga |
Kwa sababu hiyo, haikuwa ajabu Nicolas Kabipe alipoisawazishia Polisi dakika ya 60 kufuatia kazi nzuri ya kiungo Bantu Admin, aliyekuwa akiisumbua ngome ya Simba SC leo.
Kufa kwa safu ya kiungo ya Simba SC kulimfanya hata mshambuliaji Mombeki akose watu wa kumtengenezea nafasi za kufunga kipindi cha pili.
![]() |
| Kazi bado wanayo; Kocha Mkuu wa Simba SC, Alhaj Abdallah Athumani Seif 'King Kibaden' kushoto na Msaidizi wake, Jamhuri Mussa Kihwelo 'Julio' baada ya mechi wakionekana kutofurahishwa na matokeo |

.png)