• HABARI MPYA

    Saturday, August 03, 2013

    SAMATTA APIGA BAO LEO MAZEMBE IKIUA 3-0 AFRIKA

    Na Prince Akbar, IMEWEKWA AGOSTI 3, 2013 SAA 4:00 USIKU
    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ameendelea kung’ara katika michuano ya Afrika baada ya leo kuisaidia klabu yake, TP Mazembe kuifunga FUS Rabat ya Morocco mabao 3-0 katika mchezo wa Kombe la Shirikisho uliofanyika kwenye Uwanja wao mjini Lubumbashi.
    Samatta kushoto akiwa na Tressor Mputu

    Ushindi huo, unaipeleka timu hiyo ya DRC kileleni mwa Kundi B kwa kufikisha pointi nne baada ya kucheza mechi mbili na mbali ya Samatta, mabao mengine yalifungwa na Solomon Asante wa Ghana na Cheibane Traore wa Mali.
    Mchezo ujao, Mazembe itasafiri hadi Tunisia kuifuata CA Bizertin Agosti 17, wakati FUS itakuwa mwenyeji wa ES Setif ya Algeria siku hiyo hiyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: SAMATTA APIGA BAO LEO MAZEMBE IKIUA 3-0 AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top