IMEWEKWA AGOSTI 2, 2013 SAA 2:07 ASUBUHI
JANA tulisoma kuhusu mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Ngassa anavyojiandaa kwa maisha baada ya soka na leo tutaona kuhusu kiungo wa kimataifa wa Ghana, Sulley Muntari.
JANA tulisoma kuhusu mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Ngassa anavyojiandaa kwa maisha baada ya soka na leo tutaona kuhusu kiungo wa kimataifa wa Ghana, Sulley Muntari.
Nyota huyo wa zamani wa Portsmouth amefungua kampuni ya kukodisha magari ya kifahari na pikipiki kwa mastaa mbalim bali nchini Italia.
Ndinga zake: Sulley Muntari anatoa ofa hizi kwa wanasoka wenzake
Bado anacheza: Kiungo wa AC Milan alikuwa Amerika kwa ajili ya mechi za kujiandaa na msimu na alicheza dhidi ya Manchester City Jumatano
Huduma: Muntari anatoa vitu kama hivi kwa wanamuziki wabunfu na wanasoka
Mwana familia: Kaka wa Sulley, Muniru akisaini autograph
Muntari ameanzisha kampuni ambayo inaitwa 4FKMotosport, yenye maskani yake Italia ambayo inatoa huduma kwa pia wabunifu, wanamuziki na mamilionea wowote.
Akiwa ana umri wa miaka 28 tu, mitatu zaidi ya Ngassa, nyota huyo wa Ghana amejiimarisha kiuwekezaji katika kuelekea kwenye maisha baada ya soka.
Kampuni nzuri: Muntari ameweka pia bango la jezi za klabu kongwe za Italia - Inter na AC Milan
Nikumbuke mimi: Sulley ameweka picha yake ofisini kwake
Muntari amechezea klabu zote kubwa Milan, Inter na AC na alikuwa sehemu ya kikosi cha Jose Mourinho kilichotwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2010.
Ameichezea mechi 77 Ghana, na alicheza kwa muda mfupi Sunderland na kushinda Kombe la FA alipokuwa Portsmouth mwaka 2008.
Pati la ubingwa: Muntari (kushoto) alipata mafanikio alipokuwa Portsmouth kwa kutwaa Kombe la FA mwaka 2008