• HABARI MPYA

    Friday, August 02, 2013

    LIVERPOOL KUSAJILI STRAIKA BABU KUBWA NA BADO YASIZTIZA SUAREZ HAONDOKI, ARSENAL WANALO HILO!

    IMEWEKWA AGOSTI 2, 2013 SAA 1:47 ASUBUHI
    KLABU ya Liverpool imeanza harakati za kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid, Diego Costa mmoja kati ya wachezaji ghali katika historia yao.
    Wamepeleka ofa ya Euro Milioni 25 (Pauni Milioni 21.85) kumnasa Costa, wakilenga kumfanya mwanasoka huyo wa kimataifa wa Brazil kuwa mchezaji babu kubwa zaidi waliyemsajili majira haya ya joto. Atletico sasa wanatafakari ofa hiyo.
    Liverpool imekataa kusema lolote kuhusu mpango wa kumsajili Costa, mshambuliaji wa nguvu mwenye urefu wa futi 6 na inchi 2.
    Targeted: Atletico Madrid's Diego Costa could become Liverpool's latest signing
    Anayetakiwa: Nyota wa Atletico Madrid, Diego Costa anaweza kutua Liverpool
    Iwapo dili hilo litakamalika, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ataingia kwenye orodha ya wachezaji wa ghali wa klabu hiyo, akina Andy Carroll aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 35, Fernando Torres Pauni Milioni 26 na Luis Suarez Pauni Milioni 22.8.
    Brendan Rodgers anafanya jitihada za kuimarisha safu ya ushambuliaji ya Liverpool– lakini si kwamba usajili wa Costa utafungua milango ya Luis Suarez anayetakiwa na Arsenal kuondoka.
    Rodgers anataka ushindani pale mbele mwanzoni mwa msimu na haswa ikizingatiwa Suarez atakuwa anatumikia adhabu katika mechi sita za mwanzoni na Daniel Sturridge, ambaye hajacheza mechi yoyote ya kirafiki ya Liverpool anaendelea kupata ahueni maumivu ya kifundo cha mguu. 
    Staying put? Liverpool insist they are not preparing for the exit of Luis Suarez
    Anabaki? Liverpool imesistiza Luis Suarez haondoki
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: LIVERPOOL KUSAJILI STRAIKA BABU KUBWA NA BADO YASIZTIZA SUAREZ HAONDOKI, ARSENAL WANALO HILO! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top