IMEWEKWA AGOSTI 18, 2013 SAA 8:27 MCHANA
KOCHA Arsene Wenger bado anajiona hastahili lawama licha ya kipigo cha mabao 3-1 ambacho Arsenal ilichapwa na Aston Villa jana, akisema kulikuwa kuna uwezekano wa kushinda mechi hiyo.
KOCHA Arsene Wenger bado anajiona hastahili lawama licha ya kipigo cha mabao 3-1 ambacho Arsenal ilichapwa na Aston Villa jana, akisema kulikuwa kuna uwezekano wa kushinda mechi hiyo.
Lakini kocha wa The Gunners amesema hata asingejisumbua kabisa kutumia fedha kusajili majira haya ya joto kama licha ya kuandamwa na tatizo la majeruhi, damu changa ingemuwezesha kukimbizana Top Three.
Wenger pia aliamua kumtupia lawama refa Anthony Taylor - ambaye alimtoa nje kwa kadi nyekundu, Laurent Koscielny - akisema kwamba kulikuwa na matatizo ya uamuzi juu ya tukio lake.
VIDEO Kaangalie Arsene Wenger akizungumza baada ya mechi
Majuto mjukuu: Wenger alijiona yuko sahihi licha ya kufungwa 3-1
Olivier Giroud alitangulia kuifungia Arsenal mapema, lakini wakamruhusu Christian Benteke kufunga mawili na baadaye Luna kukamilisha ushindi wa wageni kwa bao la tatu.
Bosi aliloweshwa Uwanja wa Emirates baada ya dakika 90, lakini kocha huyo alifurahia kiwango cha timu yake.
"Tungeweza kushinda hii mechi, kulikuwa kuna dalili nzuri za kutosha upande wetu. Hicho ndicho tunachotakiwa kuangali,"alisema Wenger.
"Ni masikitiko makubwa, kwa sababu tulianza mchezo vizuri na ghafla mambo yakatugeukia.
"Hata tulipobaki 10 tulikuwa na nafasi ya kupata 2-2. Tungeshinda mchezo huo na wachezaji pungufu uwanjani? Nasema ndio,".
Mpweke: Wenger amesema kipigo cha jana hakikusababishwa na kutowekeza na amesema anaweza asitumie fedha.
Na Wenger amesistiza kipigo hicho katika siku ya kufungua msimu hakikutokana na kutowekeza. "Ikiwa hatujatumia fedha, ni kwa sababu hatujapata wachezaji," alisema.
"Mimi sifanyi kazi hii peke yangu, tupo timu tunaofanya kazi hiyo na tupo tayari kununua mchezaji iwapo tutapata wachezaji wazuri wa kutufaa.
"Kazi yangu ni kuwafurahisha mashabiki, lakini hatukupoteza mechi kwa sababu hiyo (ubakhili).
"Tunaichukulia kazi yetu kwa umakini wa hali ya juu na tunamchunguza kila mchezaji duniani na tunatumia saa 24 kwa siku kufanya hivyo. Tuko tayari kutumia fedha, lakini hadi tununu wachezaji, tunatakiwa kushinda michezo na si sababu ya kutoshinda mechi,".
Toa fedha: Shabiki la Arsenal likipeleka ujumbe wa moja kwa moja kwa Wenger
Wenger anaingia katika mchezo wa kuwania kucheza hatua ya makuindi ya Ligi ya Mabingwa Afrika Jumatano ugenini dhidi ya Fenerbache ya Uturuki, akiwa anakabiliwa na tatizo katika safu ya ulinzi.
Keiran Gibbs alilazimika kutoka nje baada ya dakika 28 huku akitokwa damu kichwani - na afasi yake kuchukuliwa na Carl Jenkinson - akimuongezea maumivu ya kichwa Wenger wakati anajiandaa kwenda Uturuki.
Tayari anawakosa Nacho Monreal na Thomas Vermaelen katika safu ya ulinzina kuumia kwa Gibbs kunamaanisha klabu sasa inabakiwa na wachezaji 14 wakubwa walio fiti.
"Tumepata matatizo kadhaa juu ya kurejea kwa wachezaji (walioumia) kwa ajili ya mechi ya Jumatano," alisema Wenger kabla ya kumuwakia Mwandishi: "Umepata unachokitaka, uwe na furaha. Kabla ya kuanza msimu ni hayo yote ambayo umekuwa ukiandika gazetini, sasa unatarajia nini?".