Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidy Meckysadik akiburudika na kinywaji wakati wa hafla hiyo
“Kutakwepo na kliniki za soka ambazo zitaongozwa na makocha kutoka Klabu ya Barcelona na kuna uwezekano timu itakayoibuka bingwa katika mchezo wa soka itakayoandaliwa na bia ya Castle kusafiri kwenda Camp Nou nchini Hispania kucheza mechi ya kirafiki,” alisema.
Goetzsche alisema bia ya Castle Lager imeingia mkataba wa miaka mitatu wa ushirikiano na Klabu ya Barcelona Julai 26 mwaka huu ambapo bia hiyo bora Afrika ndiyo mdhamini mkuu wa vigogo hao wa Ulaya na duniani barani Afrika.
Alisema ushirikiano huo haulengi tu biashara na wateja wao mbali jamii yote ambayo bidhaa yao inawafikia lengo likiwa ni kukuza soka.
Mgeni rasmi katika shughuli hiyo alikuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara ambaye alisifu bia ya Castle Lager kwa kupiga hatua moja mbele kutokana na kushirikiana na Klabu ya FC Barcelona kuendeleza soka la humu nchini. Dk Mukangara alisema ushirikiano huo umekuja wakati mwafaka ambao Tanzania imekuwa ikitilia mkazo kukuza na kuendeleza vipaji vya soka katika taasisi mbalimbali na akademi chache ambazo hazina miundombinu stahiki.
“Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, napenda kuwashukuru Castle Lager kwa kutusaidia na ninaamini hii itasaidia kuendeleza soka la humu nchini,” alisema.
Dk Mukangara aliongeza kuwa ushirikiano kati ya Castle Lager na Klabu ya FC Barcelona iliyosheheni wachezaji nyota kama vile Lionel Messi, Neymar na Andres Iniesta itakuwa changamoto katika kubadilisha maisha ya wachezaji wa soka Tanzania.
Waziri huyo alihakikisha kufanya kazi kwa karibu na Castle Lager kuwawezesha jamii nchini kote kupitia mchezo wa soka.
“Napenda kutoa wito kwa wanasoka wote Watanzania na wataalamu wa soka kukumbatia fursa hii inayotolewa kwa ushirikiano wa Castle Lager na Klabu ya Barcelona kutimiza programu zilizoainishwa kwenye mkataba kwa manufaa ya soka letu,” alisema Dk Mukangara.
Miongoni mwa walikwa katika uzinduzi huo walikuwa Balozi wa Hispania nchini Tanzania, Luis Manuel Ceuesta Civis, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik, Meya wa Ilala Jerry Slaa na Mkurugenzi wa Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Leonard Thadeo. |