"Mwali" Kombe la Kagasheki Cup 2013 walilotwaa Bilele FC
Timu ya Bilele FC maarufu kama KM 0 imeibuka kidedea baada ya kuilaza timu ya Rwamishenye FC leo walipopambana vikali katika fainali ya kugombea kombe la KAGASHEKI CUP 2013 iliyochezwa kwenye uwanja wa Kaitaba Bukoba mjini
Timu hizo mbili zilitoshana nguvu ya bila kufungana katika dakika tisini za kawaida na hata baada ya dakika zaidi thelathini kuongezwa hakuna aliyefanikiwa kuona lango la mwenziye na hivyo mechi hiyo kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti.
Mshindi wa pili ni Rwamishenye fc na wa tatu ni Kitendaguro(Makhirikhiri) baada ya kuwachabanga mabao 3-1 timu ya Kashai Fc juzi jioni. Wote walipewa zawadi zao kama zilivyokuwa zimepangwa.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki (kulia) ambae ndie mdhamini mkuu wa ligi hii akiteta na umati mkubwa wa mashabiki waliokusanyika uwanjani hapa
Baada ya kipa wa Bilele kudaka mkwaju wa penati wa mwisho, wachezaji wa Bilele wakikimbia kumpongeza kipa wao