IMEWEKWA AGOSTI 7, 2013 SAA 2:42 USIKU
KLABU ya Arsenal ipo katika mbio za kupambana na muda kumsajili Luis Suarez kuelekea mchezo wao wa kufuzu Ligi ya Mabingwa na kocha Arsene Wenger amesema wapo 'tayari tayari' kwa uhamisho wa mshambuliaji huyo Liverpool.
The Gunners iliweka mezani ofa ya Pauni Milioni 40, ambayo ilikuwa inaamika itatosha kwa uhamisho wa nyota huyo wa Uruguay - lakini ikapigwa chini na klabu hiyo ya Anfield.
Pamoja na hayo, Suarez ameweka wazi kwamba anataka kuondoka, akilalamika katika mahojiano kwamba Liverpool imekiuka ahadi ya kocha Brendan Rodgers.
VIDEO Luis Suarez amezingirwa na mashabiki wa Liverpool
Macho yote kwake: Suarez akipigwa picha na mashabiki alipokuwa akielekea kiruo cha watoto cha 'Take a Peek' 3D huko St Helens
Mikono: Suarez akisalimiana na mashabiki watoto nje ya kituo hicho
Katika kliniki: Suarez alizingirwa baada ya kuondoka katika kliniki hiyo
Pozi: Suarez alisimama kupiga picha na mashabiki
Mimi tu: Wachezaji wenzake Suarez wamekwenda Norway, wakati yeye anafanya mazoezi peke yake Melwood na binti yake
NUKUU NZITO YA SUAREZ
'Nina miaka 26. Nataka kucheza Ligi ya Mabingwa. Nimesubiri mwaka mmoja na hakuna hata mmoja anayeweza kusema sikujitolea kitu kitu kusaka nafasi hiyo.'
'Nina maneno ya klabu na tuliandikiana Mkataba na tutafurahi kulifikisha hili suala Bodi ya Ligi Kuu ili waamuwe kesi hii, lakini sitaki hayo yafike huko.'
'Walinipa maneno yao mwaka uliopita na sasa nataka waheshimu hayo. Na hii si kitu ambacho kinamuhusu kocha, lakini kitu ambacho kiliandikwa kwenye Mkataba. Siendi klabu nyingine kuiumiza Liverpool.'
GONGA HAPA USEMI HABARI KAMILI
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 - kwa sasa anatumikia adhabu ya kukosa mechi 10 kwa kumng'ata mchezaji wa Chelsea, Branislav Ivanovic mwishoni mwa msimu uliopita bado hajawasilisha barua rasmi ya kuondoka au kufungua mashitaka Bodi ya Ligi Kuu kushinikiza kuondoka.
Kwa vyovyote Arsenal inatakiwa kuharakisha uhamisho wa Suarez kabla ya mechi zaio mbili za kufuzu Ligi ya Mabingwa baadaye mwezi huu, kwani tarehe ya mwisho ya usajili wa michuano hiyo kwa mujibu wa UEFA ni saa 5:00 asubuhi Jumatatu ya Agosti 12.
Wenger amesema katika mahojiano na Al Jazeera Sport kwamba wanatakiwa kukimbizana na muda kuwahi dirisha la usajili kabla halijafungwa.
"Kwa sasa mambo yako tayari tayari. Nimesikia kwamba (Suarez anataka kuchukua hatua za kisheria kushinikiza uhamisho), lakini haya ni mambo ambayo wakati mwingine wewe mnunuzi huwezi kujihusisha nayo," alisema.
"Hiyo hadithi baina ya Suarez na Liverpool na sijui amesema nini, nini aliahidiwa na kipi kiliandikwa na hiyo ni Suarez na Liverpool ambao wanaweza kuamua.
"Hatuna cha kufanya. Tumeambiwa kwamba mchezaji anataka kuondoka Liverpool na hiyo ndiyo sababu tumechukua hatua. Hakika sifahamu Liverpool wataamua nini," alisema.