IMEWEKWA SEPTEMBA 7, 2013 SAA 6:46 USIKU
ENGLAND imeifumua Moldova 4-0 katika mechi ya kuwania tiketi ya kucheza Kombe la Dunia mwakani Brazil, lakini imepata pigo, Danny Welbeck aliyefunga mabao mawili ataukosa mchezo ujao dhidi ya Ukraine baada ya kupewa kadi ya njano na refa Ivan Kruzliak wa Slovakia
Welbeck alipewa kadi hiyo kwa kosa la kuendelea kucheza licha ya maelekezo ya refa kumkataza na sasa atakosekana Jumanne England ikimenyana na Ukraine.
Leo alicheza vizuri akishirikiana na Rickie Lambert pale mbele ambao wote walifunga pamoja na Steven Gerrard.
Mshambuliaji huyo wa Southampton, Lambert alitoa pasi nzuri zote za mabao ya Welbeck aliyefunga dakika za 45 na 50 na yeye mwenyewe alitangulia kufunga dakika ya 26 baada ya Gerarrd kufunga la kwanza dakika ya 12.
Kikosi cha England kilikuwa: Hart, Walker, Cole/Baines, dk45, Cahill, Jagielka, Gerrard, Walcott, Lampard, Wilshere/Barkley, dk59, Welbeck na Lambert/Milner, dk70.
Moldova: Namasco, Armas, Golovatenco, Epureanu, Bulgaru/Suvorov, dk57, Bordiyan, Ionita/Onica, dk19, Antoniuc, Dedov, Gheorghiev/Pascenco, dk84 na Sidorenco.
Zidisha mara mbili fedha zako: Welbeck amefunga mabao mawili na kuiwezesha England kupanda kileleni mwa kundi
Nyavuni: Welbeck akiifungia England bao la nne ambalo lilikuwa la pili kwake
Njano mbaya: Welbeck amepewa kadi ya njano na refa Ivan Kruzliak sasa ataukosa mchezo wa Jumnne na Ukraine
Hafuragii: Welbeck akibishana na refa baada ya mechi
Hapa ni namna ambavyo Welbeck alivyofunga bao lake la pili kwa England na la nne katika mchezo huo- sasa gonga hapa kujua zaidi yaliyojiri katika mechi hiyo
Kuongoza kwa mifano: Steven Gerrard akipiga shuti kufunga
Alifungua biashara vizuri: Steven Gerrard aliifungia bao la kwanza England
11 Bora: Rickie Lambert akishangilia bao lake aliloifungia England
Welbeck akimzunguka kipa kabla ya kufunga bao la tatu
Barkley amecheza: Kiungo kinda wa Everton aliichezea England mechi ya kwanza leo
Jack Wilshere alicheza karibu saa nzima
bado yuko sawa: Frank Lampard ameifungia England

Katima mchezo mwingine, Cristiano Ronaldo alifunga hat-trick kipindi cha pili kuipa Ureno ushindi wa 4-2 dhidi ya Ireland Kaskazini Uwanja wa Windsor Park, mechi ambayo ilishuhudiwa kadi tatu nyekundu zikitoka.
Cristiano Ronaldo akishangilia moja ya mabao yake


.png)