• HABARI MPYA

    Monday, September 09, 2013

    HATIMAYE KIGGI MAKASSI AENDA INDIA LEO KWA MATIBABU

    Na Princess Asia, IMEWEKWA SEPTEMBA 9, 2013, SAA 8:55 MCHANA
    KIUNGO wa Simba SC, Kiggi Makassi anatarajiwa kuondoka leo saa 11:00 jioni kwenda nchini India kwa matibabu ya goti, aliloumia katikati ya msimu uliopita. 
    Kiggi aliumia akiichezea Simba SC katika mchezo wa kirafiki, katikati ya msimu dhidi ya CDA mjini Dodoma na tangu wakati huo amejaribu kupata tiba za nyumbani, bila mafanikio.
    Safari India; Kiggi Makassi anakwenda kutibiwa

    Kuona hivyo, Simba SC ikaandaa mechi maalum dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar wiki iliyopita kukusanya fedha za kumpeleka mchezaji huyo India.
    Kiggi alisajiliwa na Simba SC msimu uliopita kutoka kwa mahasimu wa jadi, Yanga SC na pamoja na kuwa na mwanzo mzuri, mwanzoni mwa msimu uliopita, lakini katikati ya msimu aliumia na tangu wakati huo amekuwa nje.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: HATIMAYE KIGGI MAKASSI AENDA INDIA LEO KWA MATIBABU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top