• HABARI MPYA

    Monday, September 09, 2013

    COASTAL UNION YAIFUNZA MAFUNZO...PANDE LA BANKA LUTIMBA AMALIZA KAZI

    Na Oscar Assenga,Tanga, IMEWEKWA SEPTEMBA 9, 2013 SAA 1:24 ASUBUHI
    BAO la dakika ya 87 ambalo lililofungwa na Yayo Lutimba liliweza kuwapa ushindi Coastal Union kwenye mechi yao ya Kirafiki na Mafunzo ya Zanzibar mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga jana.
    Lutimba ambaye alisajiliwa na Coastal Union akitokea URA ya Uganda na aliyeingia kipindi cha pili aliweza kutumia vema pasi ya Mohamed Banka na kuweza kufanikisha kufunga bao hilo ambalo liliwafanya mashabiki wa soka mkoani hapa kulipuka kwa shangwe.
    Kikosi cha Coastal Union jana Mkwakwani

    Mchezo huo wa jana ulikuwa mkali wenye upinzani mkubwa kutokana na timu zote kuonekana kuukamia,huku Coastal Union wakikosa kosa mabao kwenye mechi hiyo ambapo mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna timu iliyoweza kuona lango la mwenzie.
    Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo kila timu iliweza kuingia uwanjani hapo ikiwa na hari kwa timu zote kufanya mabadiliko kwa Coastal Union kuwatoa Othumani Tamim, Mbwana Bakari, Danny Lyanga, Soud Mohamed na Atupele Green.
    Ambao nafasi zao zilichukuliwa na Masumbuko Keneth,Mohamed Banka, Yayo Lutimba, Marcus Ndehele na Abdi Banda ambao walichukua chachu kwa kuleta ushindi kwenye kikosi cha Mafunzo na kuipa ushindi timu yao kutokana na kucheza vema.
    Coastal Union iliwakilishwa na; Said Lubawa, Mbwana Bakari, Othuman Tamim, Philipo Mugenzi, Yusuph Chuma, Razack Khalfan, Danny Lyanga, Soud Mohamed, Atupele Green, Pius Kisambale na Abdallah Othuman.
    Mafunzo; Abdallah Swamadu, Abdul Halim, Haji Abdi, Yusuph Makame, Said Mussa, Hassan Ahmada, Hamad Haji, Haji Mwambe, Sadick Habibu, Mohamed Ally na Walid Ibrahim.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: COASTAL UNION YAIFUNZA MAFUNZO...PANDE LA BANKA LUTIMBA AMALIZA KAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top