• HABARI MPYA

    Sunday, September 08, 2013

    PAMOJA NA ARSENAL KUJIVUNIA IMEPATA KIFAA...KUMBE 'UKICHECHE' ULIFANYA MESUT OZIL ATIMULIWE REAL MADRID

    IMEWEKWA SEPTEMBA 8, 2013 SAA 11:33 JIONI
    MCHEZAJI mpya wa Arsenal aliyesajiliwa kwa dau la rekodi, Mesut Ozil ametuhimiwa kujichosha mwenyewe kwa kulala na walimbwende sababu iliyofanya vigogo wa Hispania, Real Madrid waamue kumuuza.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, aliyehamia Arsenal kwa Pauni Milioni 42.5 katika siku ya mwisho ya usajili, aliambiwa na Real Madrid kuweka kazi yake ya soka mbele baada ya kuonekana kuelemewa na penzi la aliyekuwa Miss Venezuela, Aida Yespica, kwa mujibu wa gazeti la El Mundo la Hispania.
    Big-money: Ozil completed his £42.5million move to the Emirates on deadline day
    Mkwanja mnene: Ozil ametua Arsenal kwa Pauni Milioni 42.5
    Venezuelan showgirl Aida Yespica
    Aida Yespica

    Amemshika: Ozil anafikiriwa kutekwa kimapenzi na aliyekuwa Miss Venezuela, Aida Yespica ambaye amekuwa akimfuata poppote Ulaya anapokwenda kucheza

    Ozil ameripotiwa kusafiri hadi Italia kila anapopata mwanya kidogo ili kupata fursa ya kuwa na mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 31 mjini Milan au katika hoteli yake mjini Paris.
    Anakadiriwa kutumia kiasi cha Pauni 15,000 kila wiki mbili kwa ndege binafsi, inayompeleka kwa Yespica.
    El Mundo limeripoti kwamba safari za asubuhi na mapema zimezidi na kiasi cha kufikia kushusha kiwango chake cha soka.
    Controversial: Some Madrid fans and players are dismayed by the sale of Ozil
    Utata: Baadhi ya mashabiki wa Madrid wamekasirika juu ya kuuzwa kwa Ozil

    Mpenzi wake mpya, Many Capristo anafikiriwa kutaka kumfuata Uingereza ili kuwa karibu naye, lakini gazeti la The Sun le leo limeripoti kwamba amekaa ushauri wa kutafuta nyumba karibu na viwanja vya mazoezi vya Hertfordshire.
    Capristo anayetarajiwa kuwa nyota mpya katika wake na wapenzi wa wachezaji, maarufu kama WAGs - mahusiano yake na mwanasoka huyo yamepewa jina Posh na Becks wa Ujerumani.
    Ozil, mwenye asili ya Uturuki, ni Muislamu, lakini mpenzi wake amekuwa maarufu Ujerumani kwa sababu ya muziki na kudansi katika show ya Televisheni
    Mesut Ozil
    Mandy Capristo

    Penzi la nguvu: Mesut Özil na mpenzi wake mwimbaji, Mandy Capristo wanatarajiwa kuhamia London baada ya mchezaji huyo kujiunga na Arsenal akitokea Real Madrid kwa Pauni Milioni 42.5
    Together: The couple have been dating for less than a year but seem particularly loved-up
    Pamoja: Wawili hao wamekuwa kwenye wimbi la mahaba kwa zaidi ya mwaka.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: PAMOJA NA ARSENAL KUJIVUNIA IMEPATA KIFAA...KUMBE 'UKICHECHE' ULIFANYA MESUT OZIL ATIMULIWE REAL MADRID Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top