• HABARI MPYA

    Saturday, September 14, 2013

    MANJI ATUA GHAFLA MBEYA MCHANA HUU NA NIYONZIMA NA VIONGOZI WENZAKE KIBAO

    Na Mahmoud Zubeiry, Mbeya, IMEWEKWA SEPTEMBA 14, 2013 SAA 7:47 MCHANA
    MWENYEKITI wa Yanga SC, Alhaj Yussuf Mehboob Manji ametua mchana huu (Saa 7:10) mjini Mbeya kuja kushuhudia mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Mbeya City jioni ya leo Uwanja wa Sokoine mjini hapa.
    Manji ametua na viongozi wenzake kadhaa, akiwemo Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji, Isaac Chanji na Mussa Katabro pamoja na kiungo Haruna Niyonzima.
    Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji akiwasili Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Songwe, Mbeya mida hii 

    Baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe mjini hapa, Manji na timu yake walikwenda hotelini kujiandaa kwenda uwanjani. Yanga SC itakuwa na mechi mbili mfululizo za Ligi Kuu mjini hapa kuanzia leo dhidi ya timu mpya katika ligi hiyo na Jumatano dhidi ya Prisons.
    Huu wa leo utakuwa mchezo wa kwanza wa ugenini kwa Yanga na wa tatu kwa jumla msimu huu, baada ya awali kushinda 5-1 dhidi ya Ashanti United na kutoa sare ya 1-1 na Coastal Union, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Mchezo huo unatarajiwa kuchezeshwa na refa Andrew Shamba kutoka Pwani, wakati Kamisaa atakuwa James Mhagama kutoka Songea.
    Kutoka kulia Mussa Katabaro, Manji, Sanga na Chanji


    Manji na Katabaro

    Mechi nyingine za ligi hiyo leo ni kati ya Simba na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam itakayochezeshwa na refa Dominic Nyamisana kutoka Dodoma. 
    Pia Azam TV itautumia mchezo huo kwa ajili ya mazoezi (broadcast training) kwa wafanyakazi wake. Hivyo mechi hiyo haitarekodiwa au kuonyeshwa moja kwa moja.
    Amekuja pia; Haruna Niyonzima naye amewasili Mbeya mchana huu

    Mechi nyingine ni Coastal Union na Tanzania Prisons (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Ruvu Shooting na Mgambo Shooting (Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani), Oljoro JKT na Rhino Rangers (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha), Kagera Sugar na Azam (Uwanja wa Kaitba, Bukoba), na Ashanti United na JKT Ruvu (Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MANJI ATUA GHAFLA MBEYA MCHANA HUU NA NIYONZIMA NA VIONGOZI WENZAKE KIBAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top