IMEWEKWA OKTOBA 7, 2013 SAA 1:05 USIKU
KIUNGO wa Manchester United, Marouane Fellani anaweza kufanyiwa upasuaji wa kiganja cha mkono ambao utamfanya ae nje ya Uwanja hadi Desemba.
Mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 27.5 msimu huu, aliikosa mei ya Jumamosi timu yake ikishinda mabao 2-1 katika Ligi Kuu ya England dhidi ya Sunderland na atakutana na wataalamu mjini Manchester kabla ya kukutana na matabibu nchini Ubelgiji.
Atazikosa mechi za timu yake ya taifa wa kuwania tiketi ya Kome la Dunia dhidi ya Croatia na Wales, na atazikosa kwa miezi miwili mechi United katika Ligi, Kombe la Ligi na Ligi ya Mabingwa.
Lakini wakati habari ilipobandikwa katika ukurasa maalum wa facebook wa klabu ya Manchester United (Facebook page), wengine waliguswa na matatizo ya Mbelgiji huyo na kumtakia heri, lakini wengine walimkandia 'kinoma'.
Majanga: Marouane Fellaini atakutana na wataalamu mjii Manchester kabla ya kwenda kukutana na daktari wa timu ya taifa ya Ubelgiji
Taarifa hiyo ilisema: "Jumamosi, imetokea habari ya kuumia kwa Marouane Fellaini, maumivu ambayo yanaweza kumuweka nje kwa angalau wiki chache... Ungana nasi kumtakia Fellaini apone vizuri..."
Pamoja nayo, baadhi ya waliochangia habari hiyo walimkandia mchezaji huyo na kuonekana kama kufurahia hali iliyompata Mbelgiji huyo.
Mmoja alisema ilikuwa habari njema, mmoja hakika alifurahia sasa anakuwa nje na mwingine akasema; 'jambo zuri kwamba maumivu yanamuweka anakuwa nje.'
Mwingine alikwenda mbali zaidi, na mwingine akimponda kwamba mchezaji mbovu zaidi kusajiliwa Ulaya nzima msimu huu' na mwingine akatoa maoni yake kwamba; 'tunaonekana vizuri bila yeye.'
Backlash! Some of the comments left by fans on the Fellaini story
Maumivu: Fellani anaweza kuwa nje kwa wiki kadhaa kama atafanyiwa upasuaji
Akimiliki mpira: Kama Fellaini aifanyiwa upasuaji, atalazimika kuvaa kifaa maalum cha kuukinga mkono wake atakaporejea uwanjani
Kocha David Moyes alisema; "Atakwenda kukutana na wataalamu. 'Hayuko vizuri sana, lakini tutasubiri hadi Jumatatu na tutajua,".
Fellaini anaweza kuhitaji kuvaa kifaa maalum cha kukinga kifundo chake cha mkoko atakaporejea uwanjani.