• HABARI MPYA

    Sunday, October 06, 2013

    UZINDUZI WA KAMPENI YA NANI MTANI JEMBE 6/10/2013 HOTUBA YA MENEJA WA BIA YA KILIMANJARO PREMIUM LAGER, GEORGE KAVISHE

    IMEWEKWA OKTOBA 6, 2013 SAA 2:15 USIKU
    "Kwanza nachukua fursa hii kuwakaribisha na kuwashukuru kwa kuitikia mwaliko wetu na kuja hapa leo hii kwenye shughuli hii ya kuzindua kwenu kampeni mpya ya Kilimanjaro Premium Lager inayojulikana kama NANI MTANI JEMBE. Natoa shukrani za kipekee kwa Mwenyekiti wa Yanga Bw. Yusuf Manji na Mwenyekiti wa Simba, Mheshimiwa Aden Rage kwa ushirikiano wao katika kufanikisha shughuli ya leo pamoja na kutuunga mkono katika kampeni hii tunayoizindua leo hii.
    Mashabiki wa Simba na Yanga wakicheza

    Meneja wa Bia ya Kilimanjaro akihutubia Leaders leo

     Kama mnavyojua Kilimanjaro Premium Lager imekuwa mdhamini mkuu wa Simba na Yanga kwa miaka mitano sasa tangu mwaka 2008 ambapo tulisaini mkataba kwa mara ya kwanza na kuongeza tena mkataba wa miaka mitano mwaka 2011 ambao utadumu mpaka mwaka 2016. Lengo letu kubwa katika udhamini huu ni kuziimarisha Simba na Yanga ili ziendelee kuwa fahari ya Watanzania kama ilivyo bia ya Kilimanjaro Premium Lager na kuzifikisha kwenye kilele cha mafanikio. Vilevile udhamini huu ulilenga kuitangaza bia ya Kilimanjaro Premium Lager kupitia klabu hizi kongwe zenye historia kubwa katika taifa hili pamoja na mashabiki wengi zaidi kuliko klabu nyingine yoyote.
    Watanzania tuna sifa ya umoja na tuna jambo moja ambalo limetuunganisha katika makundi mawili unapozungumzia soka. Bila kujali dini wala kabila, kila Mtanzania aidha ni shabiki wa Simba au Yanga na hii ni kutokana na historia kubwa ambayo vilabu hivi vimeijenga na pia kutokana na sifa kubwa ambayo vilabu hivi vimeiletea Tanzania katika bara letu la Afrika kutokana na utani wa jadi ambao ni mojawapo ya mambo yanayotutambulisha Watanzania. Utani huu wa jadi umekuwa chachu kubwa ya maendeleo ya vilabu hivi kwa sababu unaleta msukumo wa kila klabu kuhakikisha inajiimarisha ili kushindana ipasavyo na kupata mafanikio. Vile vile utani huu wa jadi umeweza kuleta msisimko wa aina yake kati ya mashabiki.
    Kupitia kampeni ya NANI MTANI JEMBE, bia ya Kilimanjaro Premium Lager imeamua kutumia utani huu wa jadi uliopo kati ya mashabiki wa Simba na Yanga kuendelea kuwaleta pamoja mashabiki wa timu hizi kongwe na zinazopendwa zaidi hapa nchini. NANI MTANI JEMBE inazinduliwa rasmi leo na itadumu kwa siku 75 hadi Desemba 14 2013. Kama ambavyo mmeona kwenye vyombo vya habari, kabla ya uzinduzi huu siku ya leo, tumetabulisha kampeni hii kwa wafanyakazi wa TBL kwenye kiwanda cha Mwanza na kiwanda cha Arusha na vilevile tutaitambulisha kampeni hii kwa wafanyakazi wa TBL Mbeya tarehe 11 mwezi huu. Hii ni katika kuhakikisha wafanyakazi wanakuwa mabalozi pia wa kutangaza kampeni hii.
    ü  Kama nilivyosema awali, NANI MTANI JEMBE itahusisha mashabiki wa klabu za Simba na Yanga.
    ü  Kilimanjaro Premium Lager imetenga kiasi cha shilingi milioni 100 ambazo zitashindaniwa Simba na Yanga kupitia mashabiki wake.
    ü  Kampeni itakapoanza kila klabu itatengewa kiasi cha shilingi milioni 50.
    ü  Katika kipindi hicho chote mteja ambaye ni Mtani Jembe akibandua ganda la kizibo cha bia ya Kilimanjaro Premium Lager ataona namba. Ataandika jina la timu yake (SIMBA au YANGA) ikifuatiwa na namba hiyo ya kwenye kizibo kasha atatuma kwenda namba 15440 na kuipa shavu timu yake. Baada ya hapo atapata ujumbe wa kuthibitisha kwamba meseji yake imepokelewa. Kwa kufanya hivyo atakuwa amepunguza kiasi cha shilingi 1,000 kwenye akaunti ya  klabu pinzani na kuiongezea klabu yake kiasi hicho cha sh. 1,000.
    ü  Mwisho wa kampeni kama mashabiki wa Simba walipiga kura zaidi na kuichangia zaidi basi Simba itapata milioni 60 na Yanga itapata milioni 40. Na vilevile mwisho wa kampeni kama mashabiki wa Yanga walipiga kura zaidi na kuichangia zaidi basi Yanga itapata milioni 60 na Simba itapata milioni 40.
    ü  Mteja anayetuma SMS atachajiwa kiwango cha kawaida cha kutuma sms na baada ya kutuma sms atapata sms ya uthibitisho kwamba ameipigia kura timu yake na kufanikiwa kuichangia kiasi cha shilingi 1,000. Kutokana na upigaji kura wa mashabiki, akiba ya timu wanayoshabikia itakuwa ikiongezeka au kupungua kulingana upigaji kura.
    Mwisho wa kampeni fedha hizo zitakabidhiwa kwa uongozi wa kila timu kulingana na matokeo ya kura na klabu zitajiamulia namna ya kutumia fedha hizo katika miradi yake ya maendeleo.
    Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage akisaidiana na Katibu wake, Evodius Mtawala  kuvutana na viongozi wa Yanga, Mohamed Bhinda na Lawrence Mwalusako kulia


    Hapa wanachuana katika Futsall
    Kampeni ya Nani Mtani Jembe itawafikia mashabiki wote wa Simba na Yanga nchi nzima kupitia matukio mbalimbali yatakayofanyika nchi nzima na matukio hayo ni pamoja na kutembelea Matawi ya Simba na Yanga pamoja na vijiwe vya Simba na Yanga, Bar promotions, Road shows, Mabonanza ya kila wiki,  Mashindano ya Fussball (mpira wa mezani) na mambo mengine mengi ya kusisimua. Mashabiki wataweza kujishindia zawadi mbalimbali zitakazotolewa kupitia matukio haya na vilevile mashabiki watakaopiga kura wataweza kujishindia zawadi mbalimbali kila siku zitakazokuwa kwenye vizibo vya chupa za Kilimanjaro Premium Lager.
    Nyinyi kama watani wa jadi mnaozipenda klabu zenu tunawaomba muwe mabalozi wa kampeni hii ili mwishoni tuone NANI MTANI JEMBE. Asanteni sana kwa kunisikiliza.
    Sasa nauliza, NANI MTANI JEMBE?"
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: UZINDUZI WA KAMPENI YA NANI MTANI JEMBE 6/10/2013 HOTUBA YA MENEJA WA BIA YA KILIMANJARO PREMIUM LAGER, GEORGE KAVISHE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top