• HABARI MPYA

    Monday, October 07, 2013

    YANGA NA MTIBWA SUGAR YAINGIZA MILIONI 97 JANA TAIFA

    Na Boniface Wambura, IMEWEKWA OKTOBA 7, 2013 SAA 8:55 MCHANA
    MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara iliyochezwa jana (Oktoba 6 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Yanga na Mtibwa Sugar imeingiza sh. 97,557,000.
    Watazamaji waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo namba 46 lililochezeshwa na Isihaka Shirikisho kutoka Tanga walikuwa 17,313. Yanga ilishinda mabao 2-0.
    Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 23,453,748.95 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 14,881,576.27.
    Mrisho Ngassa akishangilia jana baada ya kuifungia Yanga SC bao la kwanza katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.

    Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 11,925,635.06, gharama ya kuchapa tiketi ni sh. 3,171,190 wakati gharama za mchezo ni sh. 7,155,381.04.
    Kamati ya Ligi sh. 7,155,381.04, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,577,690.52 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,782,648.18.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: YANGA NA MTIBWA SUGAR YAINGIZA MILIONI 97 JANA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top