• HABARI MPYA

    Thursday, November 21, 2013

    JACK WILSHERE AUMIA TENA, ARSENAL WAIANZISHIA FA ENGLAND KWA KUKAIDI USHAURI WA WENGER

    KIUNGO Jack Wilshere amesababisha tena mgogoro baina ya klabu yake na nchi yake, England baada ya kuumia kifundo cha mguu akiichezea timu ya taifa dhidi ya Ujerumani. 
    Uamuzi wa kumchezesha Wilshere juzi usiku umeiudhi Arsenal, kwa sababu kocha Arsene Wenger aliomba mapema kiungo wake achezeshwe katika mechi moja tu kati ya mbili za kimataifa. 
    Lakini akitoka kucheza dhidi ya Chile Ijumaa usiku, akitimiza dakika 71, Wilshere pia aliingia akitokwa benchi dakika ya 64 wakati England ikifungwa 1-0 na Ujerumani na akaumia kifundo cha mguu.
    Mwenye mpira: Jack Wilshere ameumia kifundo cha mguu akiichezea England dhidi ya Ujerumani

    Hii si mara ya kwanza Wilshere anakuwa ishu baina ya Arsenal na FA, kwani iliwahi kutokea pia wakati anachezea timu ya vijana chini ya umri wa miaka 21 kwenye michuano ya Ulaya mwaka 2011, ingawa suala hilo lilipatiwa ufumbuzi. 
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 pia ameelezea wasiwasi wake wa kukosa nafasi kwenye kikosi cha England kitakachokwenda kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwakani Brazil. 
    Jack Wilshere
    Jack Wilshere replaces Tom Cleverley
    Kutoka benchi: Wilshere aliingia kuchukua nafasi ya Tom Cleverley dakika ya 64, England ikilala 1-0 dhidi ya Ujerumani
    Up for the battle: The Arsenal midfielder also played against Chile last week
    Mpambano: Kiungo huyo wa Arsenal pia alicheza mechi dhidi ya Chile wiki iliyopita
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JACK WILSHERE AUMIA TENA, ARSENAL WAIANZISHIA FA ENGLAND KWA KUKAIDI USHAURI WA WENGER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top