• HABARI MPYA

    Monday, January 06, 2014

    IVO AMTAJA MCHAWI ANAYEMBEBA LANGONI

    Na Mahmoud Zubeiry, Zanzibar
    KIPA namba moja wa Simba SC, Ivon Philip Mapunda amesema kwamba kama yupo mchawi anayemfanya afanye vizuri langoni, basi ni Yesu.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana, Ivo alisema kwamba watu wamekuwa wakihisi taulo anayoweka langoni wakati anadaka ni ya kichawi, lakini si kweli ile ni maalum kujifuta jasho wakati anafanya kazi.
    Mimi ni wa Yesu; Ivo Mapunda akionyesha maandishi yenye ujumbe wa kumsifu Yesu katika fulana yake. Chini Ivo na kitaulo chake.

    “Popote ninapokuwa, nakuwa nalindwa na Yesu, timu yoyote nayodakia lango linakuwa salama. Uwezo wangu ni kwa nguvu zake Yesu. Na kwa uwezo wake yeye baba, nitaendelea kufanya vizuri,”alisema.
    Ivo alifika Uwanja wa Amaan, Zanzibar jana akiwa amevalia fulana yenye ujumbe wa kumsifu Yesu Kristo na akakaa jukwaani wakati Simba SC ikimenyana na KMKM ya Zanzibar na kushinda 1-0, langoni akiwa amesimama kipa mwingine ‘Mfuasi wa Yesu’, Yaw ‘Pastor’ Berko, raia wa Ghana.  
    Awali, Ivo alidaka mechi mbili za Kundi B dhidi ya AFC Leopard ya Kenya na KCC ya Uganda bila kufungwa hata bao moja.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: IVO AMTAJA MCHAWI ANAYEMBEBA LANGONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top