Na Mahmoud Zubeiry, Muscat
COASTAL Union ya Tanga imepoteza mechi ya kwanza katika ziara yake ya Oman, baada ya kufungwa na wenyeji wao, Fanja bao 1-0 kwenye Uwanja wa Fanja, eneo la Fanja mjini Muscat, Oman.
Bao pekee lililowazamisha Wagosi wa Kaya hii leo limefungwa na Mohammed Al Masuari dakika ya 17 ya mchezo huo, baada ya kufumua shuti lililowapita mabeki wa Coastal na kipa wao Shaaban Hassan Kado na kutinga nyavuni.
Coastal iliyouanza mchezo taratibu ilicharuka baada ya bao hilo na kucheza kwa juhudi kutafuta kusawazisha, lakini hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika hawakufanikiwa.
Kipindi cha pili, Cosatal ikiwatumia Haruna Moshi ‘Boban’ na Danny Lyanga katika safu ya ushambuliaji, iliendelea na juhudi zake za kukomboa bao bila mafanikio.
Fanja walicheza soka nzuri ya kitabuni na Coastal walijitahidi kukabiliana nao na kwa ujumla mchezo ulikuwa mzuri.
Dakika ya 85 Keneth Masumbuko alipoteza nafasi nzuri ya kuisawazishia Coastal, baada ya kupewa pasi nzuri ya kutanguliziwa na Boban aliyekuwa akiwasumbua mno mabeki wa Fanja, lakini akashindwa kufunga baada ya kipa Ibrahim Abdulaziz kuuwahi mpira na kudaka.
Kocha Mkenya wa Coastal, Yussuf Chippo alimtoa Atupele Green dakika ya 80 na kumuingiza Mohamed Miraj, lakini hadi kipyenga cha kuhitimisha mchezo huo kinapulizwa wageni walilala 1-0.
Huo ulikuwa mchezo wa tatu kwa Coastal katika ziara yake ya hapa tangu Januari 9 hadi 23 mwaka huu, baada ya awali kushinda 2-0 mara mbili dhidi ya Nadi Oman na Musannaa. Wanatarajiwa kuwa na mechi tatu zaidi kabla ya kurejea Tanga, dhidi ya Seeb, Al Thuwaiq na Oman Club.
Kikosi cha Coastal leo kilikuwa; Shaaban Kado, Hamad Juma, Othman Tamin, Juma Nyosso, Markus Ndeheli, Razack Khalfan, Atupele Green/Mohammed Miraj dk80, Jerry Santo, Danny Lyanga, Haruna Moshi ‘Boban’ na Keneth Masumbuko.
Fanja SC; Ahmad Al Hataki/Ibrahim Abdulaziz dk46, Mohammed Al Msalami, Abdullha Al Qasabi, Mokled Al Ragadi, Abdulkhalil Fail/Sadd Al Mukmi dk25, Mohammed Al Masuari/Ahmed Hendi dk75, Badar Al Maumani/Mohamed Al Him dk60, Abos Al Hashami/Bas Akim dk69, Fahad Al Balushi/Abdul Rabam na Eli Cisse/Filipo.

![]() |
Kipa wa Coastal, Shaaban Kado akichupa kulia mpira ukitinga kushoto kwake, bao pekee la Fanja leo |
![]() |
Mshambuliaji wa Coastal Union, Danny Lyanga akimtoka beki wa Fanja leo |
Coastal iliyouanza mchezo taratibu ilicharuka baada ya bao hilo na kucheza kwa juhudi kutafuta kusawazisha, lakini hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika hawakufanikiwa.
Kipindi cha pili, Cosatal ikiwatumia Haruna Moshi ‘Boban’ na Danny Lyanga katika safu ya ushambuliaji, iliendelea na juhudi zake za kukomboa bao bila mafanikio.
Fanja walicheza soka nzuri ya kitabuni na Coastal walijitahidi kukabiliana nao na kwa ujumla mchezo ulikuwa mzuri.
Dakika ya 85 Keneth Masumbuko alipoteza nafasi nzuri ya kuisawazishia Coastal, baada ya kupewa pasi nzuri ya kutanguliziwa na Boban aliyekuwa akiwasumbua mno mabeki wa Fanja, lakini akashindwa kufunga baada ya kipa Ibrahim Abdulaziz kuuwahi mpira na kudaka.
Kocha Mkenya wa Coastal, Yussuf Chippo alimtoa Atupele Green dakika ya 80 na kumuingiza Mohamed Miraj, lakini hadi kipyenga cha kuhitimisha mchezo huo kinapulizwa wageni walilala 1-0.
Huo ulikuwa mchezo wa tatu kwa Coastal katika ziara yake ya hapa tangu Januari 9 hadi 23 mwaka huu, baada ya awali kushinda 2-0 mara mbili dhidi ya Nadi Oman na Musannaa. Wanatarajiwa kuwa na mechi tatu zaidi kabla ya kurejea Tanga, dhidi ya Seeb, Al Thuwaiq na Oman Club.
Kikosi cha Coastal leo kilikuwa; Shaaban Kado, Hamad Juma, Othman Tamin, Juma Nyosso, Markus Ndeheli, Razack Khalfan, Atupele Green/Mohammed Miraj dk80, Jerry Santo, Danny Lyanga, Haruna Moshi ‘Boban’ na Keneth Masumbuko.
Fanja SC; Ahmad Al Hataki/Ibrahim Abdulaziz dk46, Mohammed Al Msalami, Abdullha Al Qasabi, Mokled Al Ragadi, Abdulkhalil Fail/Sadd Al Mukmi dk25, Mohammed Al Masuari/Ahmed Hendi dk75, Badar Al Maumani/Mohamed Al Him dk60, Abos Al Hashami/Bas Akim dk69, Fahad Al Balushi/Abdul Rabam na Eli Cisse/Filipo.
0 comments:
Post a Comment