• HABARI MPYA

    Friday, January 10, 2014

    YAYA TOURE MWANASOKA BORA AFRIKA KWA MARA YA TATU MFULULIZO

    Na Princess Asia, Lagos
    KIUNGO wa kimataifa wa Ivory Coast, Yaya Toure ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika kwa mara ya tatu mfululizo.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, anayeng’ara katika timu ya Manchester City ya England, alipokea tuzo yake ya mafanikio ya mwaka 2013 katika usiku wa utoaji tuzo hizo za Shirikisho la Soka Afrika (CAF), jana mjiniLagos, Nigeria.
    Ameibuka kinara dhidi ya mchezaji mwenzake wa Ivory Coast, Didier Drogba na John Obi Mikel wa Nigeria. Toure, aliyeshinda tuzo hiyo mwaka 2011 na 2012, alipata kura 373 dhidi ya 265 na 236 za Mikel na Drogba waliomfuatia.
    Mfalme wa Afrika; Yaya ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika kwa mara ya tatu mfululizo

    Mshindi amepatikana baada ya kura zilizopigwa na makocha wakuu au Wakurugenzi wa Ufundi wa vyama na mashirikisho ya soka wanachama wa CAF.
    Sherehe hizo zilihudhuriwa na Maofisa mbalimbali wakiwemo Rais wa CAF, Issa Hayatou, Gavana wa Lagos, Babatunde Fashola Raji Fashola, Waziri wa Vijana na Michezo Nigeria, Alhaji Bolaji Abdullah, Wajumbe wa Kamati Kuu ya CAF na wengineo.
    Kwa tuzo ya mchezaji bora anayecheza Afrika, kiungo wa Misri, Mohamed Aboutrika aliwashinda wapinzani wake, Ahmed Fathy Mmisri mwenzake anayecheza naye Al Ahly na Mnigeria, Sunday Mba. 
    Hiyo ilikuwa mara ya nne, Aboutrika, ambaye alitangazakustaafu Desemba mwaka jana anashinda tuzo hiyo baada ya awali kushinda mwaka 2006, 2008 na 2012.poll of African national team coaches and technical directors.
    The master: Yaya Toure was crowned African Player of the Year for the third consecutive season
    Yaya Toure akizunguma baada ya kupewa tuzo ya tatu mfululizo ya Mwanasoka Bora wa Afrika
    Fireworks: Manchester City star Toure received the accolade on stage in Nigeria
    Toure akipokea tuzo yake Nigeria
    Close-up: Toure received a trophy and this specially-made plaque to commemorate the acheivement
    Toure alipokea taji na cheti hiki cha heshima kwa mafanikio yake
    Runner up: Chelsea midfielder John Obi Mikel finished second, ahead of former Blues team-mate Didier Drogba
    Kiungo wa Chelsea, John Obi Mikel ameshika nafasi ya pili mbele ya mchezaji mwenzake wa zamani Chelsea, Didier Drogba

    TUZO ZA CAF ZILIZOTOLEWA JANA:

    Mchezaji Bora wa mwaka; Yaya Toure, Ivory Coast na Manchester City
    Mchezaji bora wa mwaka anayecheza Afrika; Mohamed Aboutrika, Misri na Al-Ahly
    Mwanasoka anayechipukia; Kelechi Iheanacho (Nigeria)
    Timu bora ya mwaka; Nigeria
    Timu bora ya vijana ya mwaka; Nigeria U-17 klabu bora ya mwaka; Al-Ahly (Misri)
    Kocha bora wa mwaka; Stephen Keshi (Nigeria)
    Refa bora wa mwaka; Haimoudi Djamel (Algeria)
    Tuzo ya mchezo wa kiungwana; Mashabiki wa Nigeria
    Magwiji wa CAF; Bruno Metsu, Mehdi Faria
    Tuzo ya Platinum; Goodluck Jonathan (Rais wa Nigeria)
    11 bora wa kuunda kombaini ya Afrika;
    Kipa: Vincent Enyeama (Nigeria)
    Mabeki: Ahmed Fathy (Misri), Mehdi Benatia (Morocco), Kevin Constant (Guinea)
    Viungo: Jonathan Pitroipa (Burkina Faso), John Obi Mikel (Nigeria), Yaya Toure (Ivory Coast), Mohamed Aboutreika (Misri)
    Washambuliaji: Emmanuel Emenike (Nigeria), Asamoah Gyan (Ghana) na Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YAYA TOURE MWANASOKA BORA AFRIKA KWA MARA YA TATU MFULULIZO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top