Na Salum Vuai, Zanzibar
TIMU ya soka ya Chuoni SC, imetolewa kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho kwa jumla ya mabao 6-1 baada ya jioni hii kusalimu amri nyumbani kwa kufungwa na Howmine ya Zimbabwe mabao 2-1.
Katika mchezo huo wa marudiano uliopigwa uwanja wa Amaan, Chuoni ilianza vizuri na kupeleka mashambulizi langoni mwa wapinzani wao, na kuamsha shangwe kutoka majukwaani.
Katika dakika ya nane ya mchezo, mchezaji Bakari Ayoub aliwainua mashabiki baada ya kuifungia Chuoni bao safi, lakini kwa mshangao wa wengi, mwamuzi alilikataa kwa madai kuwa mfungaji alikuwa ameotea.
Hata hivyo, Chuoni hawakuvunjika moyo na wakaendelea kulisakama lango la wageni, na kufanikiwa kuandika bao lao katika dakika ya 12 kupitia kwa Shaaban Moka.
Moka alifunga bao hilo kufautia kosa la mlinda mlango wa Howmine Ephraem Mazarura aliyeliacha lango kuufuata mpira nje ya sanduku la 18 lakini akaambulia chenga na hatimaye Moka kukutana na mpira na bila ajizi akaachia shuti lililokwenda nyavuni moja kwa moja.
Lakini ilionekana kama kwamba kasi ya Chuoni ilikuwa sawa na nguvu ya soda, kwani dakika chache baada ya kupata bao, wachezaji walionekana kuchoka na kuanza kupoteza mwelekeo.
Hali hiyo iliwapa Howmine mwanya wa kujipanga na kuanza kucheza mpira wa kutafuta mabao na kumuweka katika wakati mgumu mlinda mlango wa Chuoni Ahmed Ali.
Mchezaji Edmore Muzarenamo nusura aipatie timu yake bao katika dakika ya 33, kama shut yake isingetoka sentimita chache nje ya goli.
Mchezaji Tembani Masulu aliisawzishia Howmine katika dakika ya 27 kufuatia wachezaji wa timu hiyo kugongeana mpira huku walinzi wa Chuoni wakishindwa kufuatana na kasi yao na kujikuta wakiruhusu nyavu zao kuchanwa.
Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko, ubao wa matokeo ulisomeka 1-1.
Kipindi cha pili Howmine walitawala mchezo na kuifunika kabisa Chuoni, na ilipofika dakika ya 80, mchezaji Kuda Musheru akaihakikishia timu hiyo ushindi baada ya kuifungia bao la pili.
Chuoni ilipata pigo katikati ya kipindi cha pili pale wachezaji wake Hamad Mshamata na Amour Omar kugongana vichwa hewani na mmoja wao kupasuka, na hivyo kushindwa kuendelea na mchezo na nafasi zao kuchukuliwa na Abdulkadir Ibrahim na Yussuf Mohammed.
Kesho KMKM itaivaa Dedebit ya Ethiopia katika mechi ya ligi ya mabingwa, ikiwa na deni a mabao 3-0 iliyofungwa Addis Ababa Februari 9, 2014.

![]() |
| Wachezaji wa Chuoni na Howmine wakionyeshana kazi leo |

.jpg)

.png)
0 comments:
Post a Comment