• HABARI MPYA

    Saturday, February 15, 2014

    LOGARUSIC ALIVYOSETEA KITAMBI CHA MWAMBUSI LEO SOKOINE

    Kocha wa Simba SC, Mcroatia Zdravko Logarusic amekuwa na desturi ya kuwatania makocha wenye vitambi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, lakini leo alibakia kukitazama namna hii kitambi cha kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi wakati timu hizo zilipokutana katika mechi ya ligi hiyo Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na kutoka sare ya kufungana bao 1-1.
    Kajificha wapi? Logarusic akimchungulia Juma Mwambusi ambaye alikaa mwisho kabisa kwenye benchi la timu yake
    Akija namchapa makonde; Kocha Juma Mwambusi leo hakutaka kukaa mwanzoni kwenye benchi la timu yake na Logarusic alipata tabu kumuona
    Kocha Juma Mwambusi ametulia tuli, kitambi chake hakikuguswa na Logarusic leo

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LOGARUSIC ALIVYOSETEA KITAMBI CHA MWAMBUSI LEO SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top