• HABARI MPYA

    Sunday, April 13, 2014

    BARCELONA YAPIGWA NA KITIMU HICHO HADI AIBU

    KLABU ya Barcelona imetimisha wiki ya machungu baada ya kufungwa bao 1-0 na Granada katika La Liga na kujiweka katika mazingira magumu ya kutetea ubingwa, siku chache baada ya kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya. 
    Bao la mapema la Yacine Brahimi lilitosha kuwalizaa tena mabingwa wa zamani waq Ulaya na sifa zimuendee kipa Orestis Karnezis, aliyezuia michomo mingi akiichezea kwa mara ya pili klabu hiyo, akiwatoa kapa Lionel Messi na wenzake.  
    Barcelona inabaki na pointi zake 78 baada ya mechi 33 katika nafasi ya pili, nyuma ya vinara Atletico Madrid na wababe wao waliowatoa Ulaya, wenye pointi 79 za mechi 32, wakati Real Madrid ina pointi 76 za mechi 32 pia.
    Majanga: Barcelona imelambwa 1-0 na Granada usiku wa Jumamosi
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BARCELONA YAPIGWA NA KITIMU HICHO HADI AIBU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top