ARSENAL imetinga Nusu Fainali ya Kombe la FA baada ya kuitoa Wigan kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 Uwanja wa Wembley usiku huu.Baada ya kuitoa timu hiyo ya Ligi Daraja la Kwanza England,maarufu kama Championship, Arsenal sasa itakutana ama na Hull City au Sheffield United Mei 17 katika fainali Uwanja huo huo wa Wembley.
Ikiwa haijashinda taji lolote tangu waliposhinda Kombe la FA mwaka 2005, Arsenal ilionekana kupania kufanya vizuri leo, ingawa iliuanza mchezo vibaya.
Wigan ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 63 kupitia kwa Jordi Gomez aliyefunga kwa penalty baada ya beki wa Arsenal, Per Mertesacker kumuangusha kwenye eneo la hatari Callum McManaman.
Hata hivyo, beki huyo Mjerumani ndiye aliyeifufua Gunners katika mchezo wa leo baada ya kufunga bao la kusawazisha dakika ya 82 na mchezo ukahamia kwenye muda wa nyongeza.
Penalti mbili za mwanzo za Wigan ziliokolewa na kipa Lukasz Fabianski, kabla ya kiungo wa Arsenal, Santi Cazorla kufunga penalti ua ushindi na kuipeleka timu hiyo fainali.
0 comments:
Post a Comment