WACHEZAJI wa Manchester United, Danny Welbeck na Tom Cleverley wamepigwa picha wakicheza disko mtaani wakiwa na demu baada ya timu yao kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na Bayern Munich.
Mshambuliaji wa England, Welbeck, mwenye umri wa miaka 23, na mchezaji mwenzake, Cleverley, mwenye miaka 24, waliserebuka katikati ya Jiji la Manchester hadi saa 9 usiku jana baada ya United kutolewa kwa jumla ya mabao 4-2 usiku wa Jumatani nchini Ujerumani.
BIN ZUBEIRY inafahamu United ilirejea jana na kukutana na mapumziko ya siku 10 kwa wachezaji wake wakaweke akili sawa kabla ya safari ya Everton Jumapili ya Aprili 20.
Wazee wa kujirusha: Welbeck akizungumza na demu (kushoto) na Cleverley (kulia) akifanya vitu vyake kitaani
Usiku mwema: Cleverley akimuaga demu. Ashley Young pia alikuwepo, lakini aliondoka mapema kwa teksi
Pati la kitaani: Welbeck (kwa nyuma) na rafiki zake wakipoza machungu baada ya kutolewa Ulaya
0 comments:
Post a Comment