Na Dina Ismail, DAR ES SALAAM
KIKOSI cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kinarejea Dar es Salaam kesho kutoka Gaborone, Botswana kilipokuwa kimeweka kambi ya wiki mbili.
Stars inayofundishwa na kocha Mholanzi, Mart Nooij iliweka kambi Botswana kujiandaa mchezo dhidi ya Msumbiji ‘Mambas’, kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Morocco.
Taifa Stars na Mambas zitamenyana nyumbani na ugenini katika Raundi ya Pili kuwania kupangwa katika makundi ya kufuzu AFCON mchezo wa kwanza unatarajiwa kupigwa Julai 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Stars pamoja na kujifua vikali, ikiwa huko ilipata pia mchezo mmoja wa kujipima nguvu dhidi ya wenyeji Botswana na kufungwa mabao 4-2.
Mshambuliaji Mrisho Ngassa ambaye alikuwa Afrika Kusini kufanya mipango ya kujjiunga na klabu ya Free State Stars ya huko, ataungana na kikosi cha Nooij katika kambi ya Dar es Salaam.
Pamoja na Ngassa kufikia makubaliano na Free State, lakini biashara ilishindikana baada ya klabu yake Yanga SC kudai dau kubwa.

0 comments:
Post a Comment