Wachezaji wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kutoka kulia Khamis Mcha 'Vialli', Mrisho Ngassa na Himid Mao wakiwa mazoezini Uwanja wa Zimpeto mjini Maputo jioni ya leo, kujiandaa na mchezo wa marudiano kesho dhidi ya wenyeji Msumbiji, Mambas hatua ya mwisho kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Morocco. Stars ililazimishwa sare ya 2-2 kwenye mchezo wa kwanza na kesho kwenye Uwanja huo watahitaji ushindi wa ugenini au sare ya kuanzia mabao 3-3. Ikiwa 2-2 mshindi ataamuliwa kwa penalti. |
0 comments:
Post a Comment