• HABARI MPYA

    Monday, August 04, 2014

    WANYAMA AOKOLEWA MA POLISI, MASHABIKI WALITAKA KUMSULUBU BAADA YA KUSHINDWA KUISAIDIA KENYA AFCON

    KIUNGO Victor Wanyama aliokolewa na Polisi baada ya mashabiki wenye hasira wa timu yake ya taifa, Kenya kuvamia Uwanja kufuatia Harambee Stars kutolewa na vibonde Lesotho katika hatua za Awali za Kombe la Mataifa ya Afrika.
    Mashabiki wa Kenya walivamia Uwanja baada ya dakika ya safe ya 0-0, timu ya Wanyama ikiwa imetoka kufungwa 1-0 katika mchezo wa kwanza.
    Police waliingia uwanjani na kumuokoa Wanyama anayechezea Southampton ya England na kumsindikiza kutoka uwanjani. Kocha Adel Amrouche, alifukuzwa baada ya mechi.
    Lesotho sasa itaungana na Uganda, Botswana, Sierra Leone, Malawi, Msumbiji na Rwanda, kwenda kwenye makundi ya kuwania tiketi ya AFCON mwakani nchini Morocco

    Chupuchupu: Kiungo wa Southampton, Victor Wanyama jana aliokolewa na Polisi Nairobi
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WANYAMA AOKOLEWA MA POLISI, MASHABIKI WALITAKA KUMSULUBU BAADA YA KUSHINDWA KUISAIDIA KENYA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top